logo

NOW ON AIR

Listen in Live

CS Namwamba kuipa Harambe Stars Sh2.5m kwa kila ushindi michuano ya kufuzu WC

Waziri Namwamba aliwahakikishia wachezaji na wafanyikazi kwamba serikali ina migongo yao

image
na Radio Jambo

Habari16 November 2023 - 07:37

Muhtasari


• Kwa kila ushindi katika michuano hiyo, Namwamba alisema serikali itaipa timu hiyo kima cha shilingi milioni 2.5

Ababu Namwamba akiwaaga Harambee Stars.

Waziri wa michezo Ababu Namwamba ametoa ahadi kubwa kwa timu ya taifa Harambee Stars pindi kabla ya kupaa ndege ya kibinafsi kuelekea nchini Gabon kwa michuano ya kufuzu kombe la dunia mwaka 2026 nchini Marekani, Kanada na Mexico.

Akizungumza na kikosi cha Harambee Stars kabla ya kuwaaga rasmi, Namwamba aliwatakia kila la kheri na kuwataka kujituma kwani juhudi zao hazitakwenda bure.

Kwa kila ushindi katika michuano hiyo, Namwamba alisema serikali itaipa timu hiyo kima cha shilingi milioni 2.5

"Tumekuandalia vizuri - ndege za kukodi, posho, kila kitu. Ni wakati wa kuangaza. Toa uwezo wako wote, na kwa kila ushindi, Ksh 2.5 milioni zinawangoja!” alisema Namwamba.

Harambee Stars itacheza dhidi ya wenyeji Gabon kabla ya kupaa ndege kuingia nchini Cote d’vore kumnyenana na timu ya taifa ya Ushelisheli wikendi.

Furaha iliongezeka alipoahidi Ksh 5 Milioni kwa ajili ya kushinda katika mapambano yote mawili.

Kwa mechi za kirafiki za hali ya juu dhidi ya wazani wazito kama vile Urusi na Qatar na kambi nzuri ya makazi, timu sasa inawapa matumaini makubwa Wakenya kwamba watarejea nchini na pointi 6 muhimu katika kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kombe la dunia.

Waziri Namwamba aliwahakikishia wachezaji na wafanyikazi kwamba serikali ipo nyuma yao, akisisitiza uungwaji mkono wa Rais William Ruto.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved