logo

NOW ON AIR

Listen in Live

ManCity kuanzisha mradi wa maji safi Kenya baada ya Nairobi kupigiwa kura

Nairobi liliibuka washindi kwa kupigiwa kura nyingi na mashabiki.

image
na Radio Jambo

Habari23 November 2023 - 08:05

Muhtasari


• Kufuatia ushindi huo, Nairobi itampokea gwiji wa Manchester City atakayefanya ziara nchini.

• Na pia kutakuwa na mafunzo ya ziada kutoka kwa wakufunzi wa Manchester City katika mtaala wa Elimu ya soka na maji.

Tap ya maji

Jiji la Nairobi limeibuka mshindi katika kura za mashabiki wa spoti ambao walikuwa wanapiga kura kuteua jiji ambalo klabu ya Manchester City itaanzisha mradi wake wa kuchimba visima katika azima la kukabili tatizo la maji mitaani kupitia soka.

Mradi huo kwa jina Xylem Water Heroes Academy Project kwa kushirikiana na wakfu wa Manchester City, Cityzens Giving walizindua upigaji kura katika baadhi ya majiji teule kote duniani kuanzia Novemba 3 hadi Novemba 17.

Baadhi ya miji ambayo ilikuwa inashiriki katika upigaji kura huo ili kujishindia mradi wa kuchimbwa kwa visima ni Bangalore (India), Barranquilla (Colombia), Nairobi (Kenya), Tacloban City (Phillipines) na Washington, D.C. (Marekani).

“Tunayofuraha kubwa kutangaza kwamba Nairobi nchini Kenya, ilikuwa mradi uliopigiwa kura nyingi zaidi na imeshinda ziara maalum ya Manchester City kwenye mradi wao, ikiwa ni pamoja na kutembelewa na Legend wa Klabu na mafunzo ya ziada kutoka kwa wakufunzi wa Manchester City katika mtaala wa Elimu ya Soka na Maji,” Manchester City walitangaza kupitia tovuti yao.

Akizungumzia mafanikio ya Nairobi, Laura Brooks, Meneja wa Kikanda wa Tackle, alisema: “Tuna furaha kubwa kushinda kampeni ya mwaka huu ya Water Heroes Academy - asante kwa kila mtu aliyepiga kura Nairobi! Hii ina maana kubwa kwa Viongozi Vijana kutoka Tackle na ni ushahidi wa kazi ya ajabu wanayofanya na Xylem kuboresha usafi wa mazingira Kibera na kukomesha ukosefu wa usawa wa muda."

Kupitia mradi huu, viongozi wachanga jijini Nairobi wanatumia uwezo wa soka kutoa ufahamu wa changamoto za maji katika jamii zao na kuwaelimisha wasichana kuhusu kutumia maji safi kwa usafi wa kiafya katika kipindi chao cha hedhi.

Water Heroes Academy, inayoungwa mkono na Xylem na Cityzens Giving, ni mtandao wa kimataifa wa miradi inayoongozwa na vijana inayolenga kukabiliana na changamoto za maji katika jamii za wenyeji kwa kutumia nguvu za soka.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved