logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Hisia zatanda huku wachezaji wa Nottingham wakimfariji Kouyate kufuatia kifo cha baba yake

Nottingham walijitoa ushindi wao wa 2-3 dhidi ya Blackpool kwa kiungo wa Senegal Cheikhou Kouyate kufuatia kifo cha babake.

image
na Samuel Maina

Michezo18 January 2024 - 09:58

Muhtasari


  • • Nottingham walijitoa ushindi wao wa 2-3 dhidi ya Blackpool kwa kiungo wa Senegal Cheikhou Kouyate kufuatia kifo cha babake.
  • •Wachezaji wa Nottingham Forests walijipanga uwanjani kwa ajili ya picha wakiwa wameshika jezi yenye namba ya Kouyate, 8, na maandishi “Thinking of you Kouyate."
walitoa ushindi wao kwa mchezaji Cheikhou Kouyate.

Jumatano usiku, wachezaji wa klabu ya soka ya Nottingham Forest walijitoa ushindi wao wa 2-3 dhidi ya Blackpool kwa kiungo wa Senegal Cheikhou Kouyate kufuatia kifo cha babake.

Habari za kusikitisha za kufariki kwa Bw Bangiougou Kouyate zilitangazwa Jumatano jioni na Shirikisho la Soka la Senegal ambalo lilithibitisha kwamba kiungo huyo mwenye umri wa miaka 34 aliruhusiwa kuondoka kwenye kambi ya mazoezi ya Lions of Teranga nchini Ivory Coast ili kumruhusu kwenda kumzika mzazi huyo wake.

Baadaye Jumatano usiku, klabu ya soka ya Nottingham Forest ambayo Kouyate anachezea ilitembelea Blackpool kwa mechi ya raundi ya muondoano ya FA na kushinda 3-2. Beki Andrew Omobamidele, kiungo Danilo na mshambuliaji Chris Wood walifungia Forest katika mechihiyo iliyoendelea hadi muda wa ziada.

Baada ya kushinda mechi hiyo, wachezaji wa Nottingham Forests walijipanga uwanjani kwa ajili ya picha wakiwa wameshika jezi yenye namba ya Kouyate, 8, na maandishi “Thinking of you Kouyate.” (Uko kwenye fikira zetu Kouyate)

Klabu hiyo baadaye pia ilithibitisha kwamba ilifanya ishara hiyo kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal.

"Kwa Kouyate," kilabu ilisema.

Jumanne, iliripotiwa kwamba Kouyate alipewa ruhusa ya kurejea nyumbani Senegal kufuatia kifo cha babake mnamo Jumanne, Januari 16, 2023.

Kiungo huyo mkongwe ambaye alikuwa mchezaji wa akiba ambaye hakutumika wakati wa mchezo wa ufunguzi wa Senegal dhidi ya Gambia, alielezwa kifo cha baba yake akiwa kambini na Lions of Teranga nchini Ivory Coast.

"Rais wa Shirikisho la Soka la Senegal Bw Augustin Senghor, wajumbe wa kamati ya utendaji, kocha wa timu ya taifa ya kandanda Bw Aliou Cisse, wachezaji wa timu ya taifa ya kandanda na familia ya mpira wa miguu wana majuto na uchungu mkubwa kuwataarifu juu ya kifo cha Bw Bangiougou Kouyate, babake Cheikhou Kouyate, mchezaji wa timu ya taifa ya Senegal,” taarifa ya Shirikisho la Soka la Senegal ilisoma.

Iliendelea, "Kifo chake kilitokea Jumanne hii, Januari 16, huko Dakar. Mazishi yamepangwa kufanyika Jumatano Januari 17 katika msikiti wa Khar Yalla na kufuatiwa na maziko katika makaburi ya Musalman huko Yoff."

Kouyate aliondoka Yamoussoukro na alitarajiwa mjini Dakar siku ya Jumatano kwa mazishi ya mzazi huyo wake


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved