logo

NOW ON AIR

Listen in Live

“Mimi ni mbarikiwa” Sancho afunguka baada ya kurudisha fomu yake Borussia Dortmund

“Mbarikiwa,” Sancho aliandika X.

image
na Davis Ojiambo

Michezo22 January 2024 - 14:02

Muhtasari


  • • Katika mechi yake ya kwanza kama mchezaji wa Dortmund, Sancho aliweza kutoa asisti kwa mwenzake Marco Reus na kuchangia bao.
  • • Wikendi iliyopita, Sancho pia alichangia kupatikana kwa mkwaju wa penalti baada ya kuangishwa kisandukuni.
Jadon Sancho

Winga wa Timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Borussia Dortmund, Jadon Sancho amefunguka na kujiita ‘mbarikiwa’ baada ya kuirudisha fomu yake ya kiwango cha juu katika timu hiyo ya Ujerumani.

Sancho ambaye amerejea Dortmund wiki mbili zilizopita kwa mkopo akitokea Manchester United alikuwa hajashiriki katika mecho yoyote tangu mwezi Septemba mwaka jana.

Hili lilitokana na kutofautiana na kocha wa United, Erik Ten Hag baada ya kile alidai ni kusingiziwa na kubebeshwa msalaba wa lawama na kocha, jambo ambalo lilimfanya kocha kumtema kutoka kikosi cha kwanza.

Baada ya kufanikiwa kurejea Borussia – timu ambayo United ilimnunua mwaka 2021, Sancho alipata kushirikishwa moja kwa moja katika mecho zote na kuonesha matumaini makubwa.

Katika mechi yake ya kwanza kama mchezaji wa Dortmund, Sancho aliweza kutoa asisti kwa mwenzake Marco Reus na kuchangia bao.

Wikendi iliyopita, Sancho pia alichangia kupatikana kwa mkwaju wa penalti baada ya kuangishwa kisandukuni.

Sancho alimsihi mchezaji mwenzake amruhusu kupata nafasi ya kufunga bao lake la kwanza kwa penalti tangu ajiunge kwa mkopo kutoka Manchester United, lakini Fullkrug alikataa na kufunga.

Hata hivyo, Sancho hakuonekana kuchukizwa na kunyimwa kupiga penalty hiyo na badala yake alikwenda kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii na kusema kwamba yeye ni mbarikiwa.

“Mbarikiwa,” Sancho aliandika X.

Bila shaka tunaweza sema kwamba mchezaji huyo licha ya kukaa nje tangu Septemba, wengi walidhani kwamba ana ubutu wa kiasi kikubwa lakini ameweza kudhihirishia ulimwengu kwamba talanta yake bado ipo na makali yake yameendelea kuboreka.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved