Droo ya ligi ya Mabingwa Ulaya, Arsenal kutifua dhidi ya Bayern

The Gunners watakuwa wenyeji wa Bayern ya Ujerumani, kwenye Uwanja wa Emirates katika mechi ya kwanza.

Muhtasari

• Iwapo Arsenal na City watashinda mechi zao timu hizo  za Uingereza zitamenyana katika nusu fainali.

kombe la ligi ya mabingwa
kombe la ligi ya mabingwa

Arsenal wamepangwa dhidi ya Bayern Munich katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa, huku Manchester City wakicheza na washindi mara 14, Real Madrid.

The Gunners watakuwa wenyeji wa Bayern ya Ujerumani, ambao wana nahodha wa Uingereza Harry Kane kwenye kikosi chao, kwenye Uwanja wa Emirates katika mechi ya kwanza.

Wakati huo huo, huu ni msimu wa tatu mfululizo kwa City, ambao walishinda taji la mwaka jana, kukutana na Real katika hatua ya maondoano.

Mechi za kwanza zitasakatwa Aprili 9-10, na za pili Aprili 16-17.

Iwapo Arsenal na City watashinda mechi zao timu hizo  za Uingereza zitamenyana katika nusu fainali.

Katika mechi nyingine, washindi mara tano Barcelona watacheza na mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain, huku Atletico Madrid, walio katika nafasi ya nne kwenye La Liga, wakiwakaribisha wapinzani wa Ujerumani, Borussia Dortmund.

Nusu fainali itafanyika tarehe 30 Aprili na 1 Mei, na mkondo wa pili wiki moja baadaye tarehe 7-8 Mei.

Uwanja wa Wembley utakuwa mwenyeji wa fainali ya mwaka huu Jumamosi, Juni 1.

Droo ya robo fainali

Arsenal v Bayern Munich

Atletico Madrid v Borussia Dortmund

Paris St-Germain v Barcelona

Real Madrid v Manchester City

Droo ya nusu fainali

Atletico Madrid au Borussia Dortmund v Paris St-Germain au Barcelona

Arsenal au Bayern Munich v Real Madrid au Manchester City

Arsenal ilitinga robo fainali kwa mara ya kwanza tangu 2010 kwa kuifunga Porto kwa mikwaju ya penalti kwenye uwanja wa Emirates siku ya Jumanne.