Arsenal wamepangwa dhidi ya mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Ni pambano kubwa huku Arsenal ikitarajiwa kukutana uso kwa uso na Harry Kane kwa mara nyingine tena.
Kane ndiye mfungaji bora wa muda wote katika mechi za Derby ya London Kaskazini na anaihesabu Arsenal kama mmoja wa wapinzani wake wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Amefunga mara 14 dhidi ya The Gunners wakati wa maisha yake ya Tottenham, akifunga tu zaidi dhidi ya Leicester na Everton.
Lakini, ingawa hilo linaweza kuwatia wasiwasi mashabiki wa Arsenal, wamepewa nguvu kubwa kabla ya pambano hilo kutokea.
Hakutakuwa na wafuasi wa Bayern ndani ya Uwanja wa Emirates kwa mechi ya mkondo wa kwanza.
The Gunners watakuwa wenyeji wa mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Emirates, na mkondo wa pili mjini Munich. Lakini Uwanja wa Emirates utajaa mashabiki wa Arsenal pekee.
Hiyo ni kwa sababu UEFA imewapa mashabiki wa Munich marufuku ya kurusha moto uwanjani wakati wa mechi yao ya 16 bora dhidi ya Lazio. UEFA iliwapa Bayern faini ya Euro 40,000 mwezi Oktoba kwa kufanya hivyohivyo.
Baada ya hapo, UEFA ilisema ikitokea tena, mashabiki wa Bayern hawakuweza kununua tikiti kwa mchezo wa ugenini. Na ndicho kilichotokea sasa, kuipa Arsenal faida kubwa.