logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ten Hag aahidi kushinda fainali ya FA

Kocha mkuu wa Manchester United amewaahidi mashabiki ushindi wa kombe la FA.

image
na Davis Ojiambo

Michezo16 May 2024 - 07:32

Muhtasari


  • • Ten Hag awahakikishia mashabiki wa United ushindi wa kombe la FA.
  • • Fainali ya kombe la FA  kuchezwa Jumamosi 25, Mei 2024 ugani Wembley.

Kocha mkuu wa Manchester United ,Eric Ten Hag ana imani kubwa timu yake itashinda kombe la FA . Ten Hag alisema haya baada ya ushindi wa nyumbani wa 3-2 dhidi ya Newcastle usiku wa Jumatano ,kwenye pambano la ligi kuu ya Uingereza.Kobbie Mainoo, Amad Diallo na Rasmus hojlund walicheka na wavu kila mmoja .

Kwenye mazungumzo na wanahabari baada ya mechi , Ten Hag aliwamiminia sifa mashabiki huku akiwaahidi wachezaji wake watafanya juu chini ili kuleta kombe la FA nyumbani .

'Ninawaahidi kwamba wachezaji watafanya kila kitu ili kuleta kombe hapa Old Trafford...' alisema Ten Hag

Manchester United itachuana na Manchester City kwenye fainali ya kombe la FA Jumamosi 25, Mei 2024 ugani Wembley. Manchester City ambao ni mabingwa watetezi wameshinda kombe hilo mara saba na pia watakuwa kwenye mishemishe za kusaka ubingwa huo kwa mara nyingine.

Aidha ni fursa nyingine kwa Ten Hag kujiliwaza baada ya kuwa na fomu mbaya ligini.Ikiwa watanyakuwa kombe hilo , basi watakuwa wamejihakikishia nafasi kwenye mashindano ya bara Ulaya, msimu ujao.

Je , Ten Hag ataweka furaha kwa nyuso za wana Manchester?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved