Kandarasi ya Salah akiwa Liverpool inaisha Juni 2025 na kumekuwa na nia ya pesa nyingi kutoka Saudi Arabia.
Alikuwa chini ya ofa ya pauni milioni 170 kutoka kwa Al-Ittihad mwaka jana. Vilabu vya mashariki ya kati vinatazamiwa kurejea tena kwa ajili yake msimu huu wa joto, huku uvumi ukidai kuwa wako tayari kulipa rekodi ya dunia ya £200m kwa nyota huyo.
Baada ya msimu kumalizika Jumapili, Salah alichapisha picha kwenye mitandao ya kijamii akiwa kwenye uwanja wa Anfield akiwa na binti zake wawili Makka mwenye umri wa miaka 10 na Kayan, 4.
Salah alituma ujumbe wa kuaga Klopp licha ya mzozo kati ya wawili hao huko West Ham mnamo Aprili 27, ambao ulisomeka:
"Ilikuwa nzuri kushiriki nawe mataji na uzoefu huo wote kwa miaka saba iliyopita. Nakutakia mafanikio mema kwa siku zijazo na natumai tutakutana tena."
Salah kisha akafuatia na chapisho lingine ambalo lilionekana kuashiria kusalia Liverpool kwa msimu ujao, aliandika:
"Tunajua kwamba mataji ndiyo yana umuhimu na tutafanya kila linalowezekana ili hilo lifanyike msimu ujao. Mashabiki wetu wanastahili na tutapigana kama kuzimu."
Arne Slot, ambaye alithibitishwa kuwa kocha mpya wa klabu hiyo,bila shaka atakuwa na matumaini kuwa Liverpool itamuweka nyota wao msimu huu. Mholanzi huyo ameripotiwa kusaini mkataba wa miaka mitatu.Na tangazo rasmi la Slot lilikuja baada ya Klopp kujaribu kuanza wimbo wa mrithi wake wakati wa hotuba yake ya kuaga baada ya Liverpool kuichapa Wolves 2-0. Klopp aliwataka mashabiki wa Liverpool kumkaribisha meneja mpya jinsi walivyo mkaribisha.
"Karibisheni meneja mpya kama mlivyonikaribisha. Unaingia ndani tangu siku ya kwanza. Unaendelea kuamini,unaisukuma timu. Mimi ni mmoja wenu sasa,nawapenda sana. "
Slot kwa upande wake,wakati wa kuaga klabu yake ya Feyenoord alisema;
"Kwa hakika sio uamuzi rahisi kufunga mlango nyuma yako kwenye kilabu ambacho umepata matukio mengi mazuri na kufanya kazi kwa mafanikio na watu wengi wa ajabu. Lakini kama mwanaspoti, fursa ya kuwa kocha mkuu katika Ligi ya Primia, katika moja ya vilabu vikubwa duniani, ni vigumu kupuuza,"