logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jeraha lamuweka Tchouameni nje ya fainali ya UEFA

Mkufunzi wa Real Madrid amethibitisha kuwa Tchouameni atakosa fainali ya UEFA kutokana na jeraha.

image
na Davis Ojiambo

Michezo24 May 2024 - 12:55

Muhtasari


  • •Hajacheza tangu apate jeraha la mguu wakati wa ushindi wao wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Bayern.
  • •Mkufunzi wa Real Madrid Carlo Ancelloti alithibitisha  kwenye mkutano na wanahabari Ijumaa 24
Aurellian Tchouameni. picha;Instagram

Kiungo wa kati wa Real Madrid Aurelien Tchouameni atakosa fainali ya Ligi ya Mabingwa kutokana na jeraha la mguu na huenda akawa na shaka kwa michuano ya Ulaya, meneja wa mabingwa hao wa la liga, Carlo Ancelotti alisema Ijumaa.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24, ambaye amecheza mechi 38 katika michuano yote akiwa na Real msimu huu, hajacheza tangu apate jeraha la mguu wakati wa ushindi wao wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa dhidi ya Bayern Munich mapema mwezi huu.

Real itamenyana na Borussia Dortmund katika fainali ya ligi ya mabingwa huko Wembley mnamo Juni 1.

"Kwa sasa anafanya mazoezi ya kibinafsi lakini hayuko tayari kwa fainali ya ligi ya mabingwa," Ancelotti aliwaambia waandishi wa habari kabla ya mchezo wao wa mwisho wa la liga dhidi ya Real Betis Jumamosi.

Tchouameni amekuwa akicheza mara kwa mara katika timu ya Ancelotti msimu huu, akikosa mechi chache tu kutokana na jeraha mnamo Novemba na Desemba. Wakati fulani amekuwa akiitwa kucheza nafasi ya beki wa kati kutokana na majeraha ya Eder Militao na David Alaba, lakini dakika zake nyingi alizipata kama kiungo mkabaji. Tchouameni ameichezea timu yake ya taifa mara 31, akifunga mabao matatu.

Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps alikuwa amemtaja Tchouameni alipotambulisha kikosi chake cha wachezaji 25 kwa ajili ya Euro wiki jana. Michuano ya Euro itaanza Juni 14 nchini Ujerumani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved