logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Man United watwaa ubingwa wa Kombe la FA

Katika pambano la fainali lilipigwa Wembley, magoli mawili ya ManUnited yalifungwa na Garnacho na Mainoo.

image
na Samuel Maina

Michezo26 May 2024 - 05:36

Muhtasari


  • •Katika pambano la fainali lilipigwa Wembley, magoli mawili ya ManUnited yalifungwa na Alejandro Garnacho na Kobbie Mainoo

Manchester United imetwaa ubingwa wa Kombe la FA kwa ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya mahasimu wao Manchester City likiwa ni taji lao la 13 mshindano hayo, taji moja pungufu ya Arsenal.

Katika pambano la fainali lilipigwa kwenye dimba la Wembley, magoli mawili ya Manchester United yamefungwa na Alejandro Garnacho na Kobbie Mainoo, huku kukiwa na goli pekee la Manchester City lililofungwa na Jeremy Doku.

Si tu kombe la FA ambalo Manchester United wamenyakua kwa ushindi huu, pia watacheza mashindano ya Ligi ya Uropa msimu ujao.

Kocha wa Man United, Erik ten Hag amelazimika kujibu maswali mengi na hakika amesikia mengi kuhusu mustakabali wake wikendi hii kwani bado hakuna uhakika iwapo atakuwepo msimu ujao hususan kutokana na kumaliza nafasi ya nane katika Ligi Kuu ya England.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved