Aubameyang avunja kimya kuhusu kuondoka Arsenal

Nyota wa zamani wa Arsenal amedokeza sababu zilizochangia kuondoka Arsenal miezi 18 iliyopita.

Muhtasari

•Mkataba wa Aubameyang ulikatizwa  miezi 18 iliyopita,baada ya kutangazwa na kocha  Mikel Arteta

•Aubameyang alisema kuwa alifokewa na Arteta baada ya kuwasili kwa kuchelewa wakati huo alikuwa  ametoka kumuona mama mzazi aliyekuwa mgonjwa.

Picha : X
Picha : X

Pierre-Emerick Aubameyang amesema Mikel Arteta alimshutumu kuwa alimsaliti wakati wa kipindi ambacho kilishuhudia maisha yake ya soka ya Arsenal yakifikia kikomo.

Nahodha huyo wa zamani wa 'The Gunners' alitimuliwa Emirates miezi 18 tu baada ya kuwasaidia  kutwaa ubingwa wa kombe la FA na kuandikisha mkataba mpya. Auba aliachwa nje ya mchezo dhidi ya Southampton mnamo Disemba 2021 na huo ndo ulkuwa mwisho wake.

Hatimaye kusitishwa kwa mkataba wake kulimruhusu kujiunga na Barcelona, ​​lakini kabla ya kuzuiliwa na Arteta, ambaye alimshutumu Aubameyang baada ya kumtembelea mama yake mgonjwa na licha ya kuidhinisha safari ya nje ya nchi.

Nyota huyo wa sasa wa Marseille kwenye mahojiano na Cointerview alisema:

"Ilikuwa katika kipindi cha COVID na tulikuwa tukicheza,dhidi ya Everton. Msimu wangu haukuwa mzuri, tulikuwa tunatatizika katika ligi na siku moja kabla ya kocha alituambia haijalishi tumeshinda au la, tuna siku ya kupumzika lakini ukitaka kuondoka, unajijulisha kabla ya mechi kwa sababu lazima ufuate sheria...'

'Mama yangu miezi michache alipatwa na ugonjwa, ilikuwa ni wakati wa Krismasi hivyo nilienda kumuona kocha na nikamwambia..Kocha, nakuja kukuona kwa sababu ningependa kuondoka, 'Naenda kumchukua mama yangu ili kumrudisha kwa ajili ya likizo.'

Aubameyang alilazimika kupitia itifaki mbalimbali za Covid, lakini alicheleweshwa kidogo kurejea Arsenal. Pia alichukua muda  kuliko ilivyopangwa na Arteta na hatimaye kuvuruga uhusiano wao.

Auba alisema kuwa baada ya kuwasili Arsenal,Arteta alimfokea kana kwamba ana kichaa.Hii ni baada ya mkutano na wachezaji wengine wa Arseanal.Huku akidai kuwa Aubameyang amemsaliti,hivo kuvuruga uhusiano wao.