logo

NOW ON AIR

Listen in Live

David Ochieng aitwa kujiunga na kambi ya Harambee Stars nchini Malawi

David Ochieng amesafiri kujiunga na kikosi cha Harambee Stars nchini Malawi.

image
na Davis Ojiambo

Michezo10 June 2024 - 08:35

Muhtasari


  • •Ochieng amesafiri kuelekea Malawi kujiunga na kambi ya Harambee Stars baada ya kupokea mwito kutoka kwa  kocha Engin Firat.
  • •Ochieng amechezea Harambee Stars mechi yake ya mwisho Juni 2023,kwenye mashindano ya mataifa manne kabla ya kutemwa nje kwenye kikosi.

David ‘Cheche’ Ochieng ambaye ni beki wa timu ya Kenya Police Fc atajiunga na kikosi cha Harambee Stars nchini Malawi baada ya kuitwa na kocha Engin Firat.

Ochieng atakuwa mchezaji wa hivi punde zaidi kujiunga na kambi kuimarisha safu ya ulinzi ya Kenya kwa mechi ya kufuzu kwa kombe la dunia 2026  dhidi ya mabingwa wa Afrika Ivory Coast itakayochezwa Jumanne katika uwanja wa kitaifa wa Bingu mjini Lilongwe.

Beki huyo amechezea Harambee Stars mechi  kadhaa hapo awali kabla ya kutemwa nje kwenye kikosi kilichosafiri kwenda Malawi. Mechi yake ya mwisho ikiwa ni Juni 2023 alipocheza katika mashindano ya mataifa manne katika mechi dhidi ya Pakistan na Mauritius.

Firat alitaja kuwa sare dhidi ya Burundi ilitokana na majeraha ambayo yanakumba kikosi chake. Beki maarufu Erick 'Marcelo' Ouma yupo mkekani pamoja na Joseph Okumu, hivo ana imani kuwa David Ochieng atakuwa anaimarisha ulinzi kwenye kikosi cha Harambee Stars.

Firat amewajumuisha wachezaji kadhaa  tangu mechi dhidi ya Burundi kukamilika,miongoni mwao wakiwa ni David Okoth kutoka klabu ya Kenya Police, Baron Ochieng anayechezea Sofapaka pamoja na Clyde Senaji anayechezea Nyasa Big Bullets nchini Malawi.

Kenya itakuwa inashuka dimbani Jumanne 11, Juni 2024 kumenyana na vigogo wa Afrika Ivory Coast kwenye mechi yao ya pili mwezi huu baada ya kukabana sare ya 1-1 na Burundi.

IKiwa Harambee stars watakosa alama tatu Jumanne, basi matumaini ya kufuzu kwa kombe la dunia yatakuwa yanadidimia kwa kuwa watakuwa alama nane nyuma ya viongozi wa jedwali, Ivory Coast.

Je,unahisi kuwa Harambee Stars watafuzu kwenye kombe la dunia 2026


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved