Euro 2024: Hali ya Mbappe sio nzuri huku Slovakia ikiishangaza Ubelgiji

Mbappe alipiga mpira kwa kichwa na uso wake ukagonga bega la Kevin Danso katika pasi ya kufuatisha.

Muhtasari

•Rais wa Shirikisho la Soka la Ufaransa, aliwaambia waandishi wa habari mjini Duesseldorf kwamba Mbappe "hahitaji kufanyiwa upasuaji", kiwango cha jeraha lake bado hakijajulikana.

Image: BBC

Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps amesema nahodha Kylian Mbappe "hayuko vizuri" baada ya kuoata jeraha baya la pua katika ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Austria Jumatatu.

Wakati Philippe Diallo, rais wa Shirikisho la Soka la Ufaransa, aliwaambia waandishi wa habari mjini Duesseldorf kwamba Mbappe "hahitaji kufanyiwa upasuaji", kiwango cha jeraha lake bado hakijajulikana.

Mwishoni mwa mchezo wa ufunguzi wa Euro 2024 wa Ufaransa mjini Düsseldorf, Mbappe alipiga mpira kwa kichwa na uso wake ukagonga bega la Kevin Danso katika pasi ya kufuatisha.

Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 25 alipokea matibabu uwanjani, akiwa na damu nyingi usoni, na kisha akatoka nje ya uwanja huku Ufaransa ikitaka kumtoa ili nafasi yake kuchukuliwa na Olivier Giroud.

Mchezo ulipoanza tena, Mbappe alienda uwanjani bila ruhusa na kuketi - hatua iliyomfanya kupewa kadi ya njano.

Nafasi yake ikachukuliwa na Giroud.

"Haendelei vizuri," bosi Didier Deschamps alisema katika mkutano wa waandishi wa habari baada ya mechi.

Image: BBC

Kwingineko Slovakia ilizua taharuki katika mechi yao ya ufunguzi ya Euro 2024 ilipowashangaza Wabelgiji katika Kundi E kwa kuwashinda bao 1-0 katika mchuano mkali mjini Frankfurt.

Kulikuwa na hali mbaya katika dakika za mwisho ambapo Romelu Lukaku alidhani alisawazisha, lakini (VAR) ikakataa bao hilo na kusema mpira ulishikwa kwa mikono wakati wa maandalizi.

Lilikuwa ni bao la pili alilofunga ambalo lilikataliwa na VAR baada ya hapo awali kuunganisha kwa kichwa mpira wa kichwa kutoka kwa Amadou Onana.

Ivan Schranz aliiweka Slovakia mbele alipotumia vyema makosa ya Jeremy Doku wa Manchester City.