logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Anthony Kimani aondoka Ulinzi stars baada kuwa kocha wa mwaka mmoja

Katika kutangaza mabadiliko hayo, uongozi wa klabu ulimshukuru Kimani kwa uongozi wake wakati alipokuwa klabuni hapo

image
na Davis Ojiambo

Michezo16 July 2024 - 09:12

Muhtasari


  • •Katika kutangaza mabadiliko hayo, uongozi wa klabu ulimshukuru Kimani kwa uongozi wake wakati alipokuwa klabuni hapo.
  • •Kimani alianza kuwa kocha mkuu na timu hio kabla ya kuanza kwa msimu uliopita na alikumbana na changamoto nyingi.

Ulinzi Stars imetangaza kuachana na kocha mkuu Anthony Kimani baada ya kuwafundisha kwa msimu mmoja pekee.

Katika kutangaza mabadiliko hayo, uongozi wa klabu ulimshukuru Kimani kwa uongozi wake wakati alipokuwa klabuni hapo.

“Tmu ya Ulinzi inapenda kutoa shukurani zake kwa Anthony Kimani kwa michango yake katika klabu wakati akiwa kocha mkuu.”

“Anthony Kimani atakuwa sehemu ya familia ya Ulinzi daima," ilisema taarifa ya klabu.

Kimani alitoa shukrani zake kwa kila mtu anayehusishwa na klabu hiyo.

"Nataka kuchukua fursa na kutoa shukrani zangu za dhati na pongezi kwa kila mmoja wenu.”

“Msimu huu uliopita umekuwa safari ya ajabu, iliyojaa changamoto, ushindi, na kumbukumbu nyingi ambazo nitahifadhi milele, "alisema.

"Wakati muda wangu hapa umekuwa mfupi, unganisho na uzoefu ambao tumeshiriki utakaa nami kila wakati.”

“Ninaamini katika uwezo wa timu hii na nina imani kuwa mambo makubwa yanawangoja nyinyi nyote.”

“Nawatakia nyote mafanikio na furaha tele, ndani na nje ya uwanja. Kwa shukrani nyingi na salamu za joto, "aliongeza.

Kimani alianza kuwa kocha mkuu na timu hio kabla ya kuanza kwa msimu uliopita na alikumbana na changamoto nyingi.

 Timu hiyo ilijihakikishia usalama wao wa kusalia katika ligi ya FKF katika siku ya mwisho ya msimu kwa ushindi wa dhidi Kariobangi Sharks.

Kocha Kimani ni mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Kenya ambaye alianza maisha yake ya ukocha katika AFC Leopards akiwa kocha msaidizi wa pili baada ya kuzichezea Mathare United na AFC Leopards.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved