Mashabiki wa Barcelona wachanga zawadi kwenye TikTok Live ya klabu kumnunua Nico Williams

Wengine walikuwa wanaweka wazi kwamba hela hizo ni kwa ajili ya kufanikisha dili ya kumnunua Nico Williams, 22, kutoka klabu ya Atletic Club ambaye kipengele chake kuachiliwa kwa euro milioni 58 ($63.2m).

Muhtasari

• Barca wamesalia kuvuka kiwango cha matumizi ya kila mwaka kilichowekwa na LaLiga, na kuwazuia kusajili wachezaji wapya, lakini Tebas alisema hali yao ya kifedha inaimarika.

NICOLAS WILLIAMS
NICOLAS WILLIAMS
Image: INSTAGRAM

Huku klabu ya Barcelona ikiwa inapitia mpito wa changamoto kihela, mashabiki wa klabu hiyo sasa wamefanya hisani na kuingia kwenye kipindi cha moja kwa moja cha klabu hiyo kwenye TikTok na kutuma zawadi kadhaa.

Mashabiki hao katika jumbe zao baada ya kutuma zawadi hizo ambazo TikTok baadae huzilipa kama hela, wengi wao walikuwa na ujumbe mmoja tu kwa klabu – kutumia hela hizo kumnunua winga Nico Williams.

Wengine walikuwa wanaweka wazi kwamba hela hizo ni kwa ajili ya kufanikisha dili ya kumnunua Nico Williams, 22, kutoka klabu ya Atletic Club ambaye kipengele chake kuachiliwa kwa euro milioni 58 ($63.2m).

Barca wamesalia kuvuka kiwango cha matumizi ya kila mwaka kilichowekwa na LaLiga, na kuwazuia kusajili wachezaji wapya, lakini Tebas alisema hali yao ya kifedha inaimarika.

Hapo awali ESPN iliripoti hamu ya Barca kusajili kiungo na winga wa kushoto msimu huu, huku Williams akipewa kipaumbele kwa jukumu la mwisho.

Winga huyo wa Athletic amecheza Euro 2024 msimu huu wa joto, na kuisaidia Uhispania kutinga fainali Jumapili dhidi ya England.

Pia amekuwa akiulizwa mara kwa mara kuhusu mustakabali wake akiwa Ujerumani jambo ambalo limeikasirisha klabu yake ya sasa.