Beki wa Manchester United,Harry Maguire amethibitisha kuwa ameambiwa kuwa yeye ni sehemu ya kikosi cha klabu hiyo na hakuna mipango yoyote kwa yeye kuondoka Old Trafford.
Kwenye mazungumzo na Sky Sports , Maguire anatazamia mustakabali wake kuendelea katika klabu hiyo baada ya kuambiwa kuwa yuko sehemu ya mipango inayoendelea Old Trafford.
"Kila kitu nilichosikia na kitendo nilichoonyeshwa kutoka kwa klabu, mimi ni sehemu ya siku zijazo na ni wakati wa kupiga hatua na kuifanya klabu hii kufanikiwa tena, twafaa kuwania mataji makubwa sasa." Maguire alisema.
Maguire, ambaye nusura aondoke katika klabu hiyo majira ya joto yaliyopita, alicheza mechi 22 za primia msimu uliopita huku United ikisajili idadi kubwa ya majeraha miongoni mwa beki wao msimu uliopita.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alikosa mechi za mwisho msimu uliopita;kwa kujumuisha fainali ya kombe la FA na Euro 2024.
Kuhusu majeraha ya msimu uliopita,Maguire alisema kuwa yalimwathiri pakubwa kisaikolojia na katika maisha yake ya soka hajawahi pitia hayo.
"Ilikuwa wakati mgumu sana katika taaluma yangu. Pengine ulikuwa wakati mgumu zaidi katika kazi yangu hadi sasa," alisema.
Aliongeza;
"Ili kujiweka katika nafasi ambayo mwaka mzima nimefanya bidii kucheza;mwisho wa msimu na kucheza katika michezo hii mikubwa, fainali za kombe na kisha kwenda kwenye Euro ...Nilihisi kama nilijiweka katika nafasi nzuri ya kimwili na kiakili kwenda na kufanya kiwango cha juu zaidi, na kukabiliana na kushindwa niliyopata kutokana na jeraha, ilikuwa wakati mgumu sana kwangu."
Maguire sasa anatazamia msimu mpya katika klabu ya Man Utd chini ya Ten Hag, ambaye hivi majuzi alisaini mkataba mpya katika klabu hiyo hadi 2026.
Manchester United wataanza msimu wao wa ligi kuu ya 2024/25 kwa mechi ya nyumbani dhidi ya Fulham, Ijumaa Agosti 16.
Je ,unahisi Maguire atapewa muda wa kucheza hasa baada ya United kumsajili beki shupavu Leny Yoro?