logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Arsenal watangaza usajili wa beki Ricardo Calafiori huku Emile Smith Rowe akiondoka

Smith Rowe anajiunga na Fulham kwa mkataba unaoripotiwa kuwa wa thamani ya £27m pamoja na nyongeza za £7m.

image
na SAMUEL MAINA

Michezo30 July 2024 - 05:08

Muhtasari


  • •Arsenal ilitoa tangazo hilo Jumatatu jioni ikifichua kuwa beki huyo mwenye umri wa miaka 22 amesaini mkataba wa muda mrefu.
  • •Smith Rowe anajiunga na Fulham kwa mkataba unaoripotiwa kuwa wa thamani ya £27m pamoja na nyongeza za £7m.

Klabu ya Arsenal imetangaza kumsajili beki wa kushoto wa Italia, Ricardo Calafiori.

Klabu hiyo yenye maskani yake jijini London ilitoa tangazo hilo Jumatatu jioni ikifichua kuwa beki huyo mwenye umri wa miaka 22 amesaini mkataba wa muda mrefu.

Dili hilo limeripotiwa kugharimu thamani ya pauni milioni 42 ($54m) na sasa atavaa jezi namba 33 kwa msimu ujao wa 2024/25.

"Mchezaji wa kimataifa wa Italia Riccardo Calafiori amejiunga nasi kutoka Bologna ya Serie A kwa mkataba wa muda mrefu. Beki huyo mwenye umri wa miaka 22 alikuwa mchezaji wa kikosi cha Azzurri kwenye Euro 2024, baada ya msimu uliojaa uchezaji wa kuvutia katika safu ya ulinzi ya Bologna," Arsenal ilisema kwenye taarifa.

Msimu uliopita, Riccardo alikuwa nguzo ya safu ya nyuma ya Bologna, akiibuka kama mmoja wa wachezaji wenye nguvu na thabiti kwenye Serie A.

Ameelezea furaha yake kujiunga na Arsenal akifichua kuwa imekuwa ndoto yake kucheza Ligi ya Premia tangu akiwa na umri wa miaka 12.

"Inashangaza lakini kwa mtazamo wangu, ni mwanzo tu, mwanzo wa kitu kikubwa zaidi, kwa hivyo ninafurahi kuanza kuichezea Arsenal," alisema.

Calafiori alitambulishwa kwa wachezaji wenzake wapya nchini Marekani siku ya Jumatatu ambapo wanaendelea na maandalizi yao ya kabla ya msimu mpya.

Usajili wake unakuja wakati kiungo Emile Smith Rowe anaondoka klabuni humo. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anajiunga na Fulham kwa mkataba unaoripotiwa kuwa wa thamani ya £27m pamoja na nyongeza za £7m.

Arsenal walikuwa wamemkabidhi Smith Rowe jezi namba 10 baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitano na klabu hiyo mnamo 2021.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved