Kiungo wa kati wa Chelsea na raia wa Argentina ,Enzo Fernandez amejiunga na wachezaji wake kule Marekani baada ya kesi yake kuhusu 'nyimbo za ubaguzi' kufungwa na Chelsea.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23, alitua Atlanta nchini Marekani usiku wa jumatatu. Vyanzo kutoka Chelsea vinaarifu kuwa aliomba msamaha pindi tu alipowasili.
Video kuhusu ubaguzi kwa wachezaji wa asili ya kiafrika , iliyotumwa kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii baada ya Argentina kuifunga Colombia 1-0 kwenye fainali ya Copa America tarehe 14 Julai ilizua utata.
Video hiyo ilikuwa na wimbo ulioimbwa na baadhi ya kikosi cha Argentina kuhusu wachezaji weusi wa Ufaransa, ambao shirikisho la soka la Ufaransa lilisema ni pamoja na wimbo unaodaiwa kuwa wa "kibaguzi na ubaguzi".
Malalamiko yalitolewa kwa shirikisho la soka duniani Fifa, huku Chelsea wakianzisha utaratibu wa ndani wa kinidhamu ambao sasa umefungwa.
Chelsea ina wachezaji saba wa Ufaransa ambao ni weusi au mchanganyiko katika kikosi chao cha kwanza. Axel Disasi, Benoit Badiashile, Lesley Ugochukwu, Christopher Nkunku, Malo Gusto na Fofana wote walikuwa sehemu ya kundi lililosafiri katika ziara ya Chelsea ya Marekani.
Beki wa kati, Wesley Fofana,alikuwa amechapisha picha ya video hiyo kwenye Instagram, akiielezea kama "ubaguzi wa rangi usiozuiliwa".
Taarifa kutoka BBC Sport ilieleza kuwa wachezaji kadhaa walifurahia mazungumzo ya awali, huku meneja mpya Enzo Maresca akitarajiwa kuthibitisha kurejea kwa kiungo huyo wa kati aliyenunuliwa kwa pauni milioni 107.
Fernandez pia amejitolea kutoa pesa kwa shirika la misaada la kupinga ubaguzi, kiasi ambacho kitalingana na Chelsea.
Noni Madueke aliunga mkono maoni hayo akisema hali "itakuwa sawa", lakini nahodha Reece James alikubali hali hiyo kama "tatizo" na akasema yuko tayari kufanya kazi kama mpatanishi.
Hata hivyo uchunguzi wa FIFA kuhusu tukio hilo unaendelea.