Familia ya nyota wa zamani wa Man Utd na Chelsea, Radamel Falcao hatimaye wapo salama baada ya kukimbizwa hospitalini baada ya kuvuta hewa iliyojaa gesi yenye sumu.
Mke wa Falcao Lorelei alieleza kuwasha hita ya maji kwa ajili ya bwawa lao la kuogelea kulisababisha kuvuja kwa gesi aina ya Carbon monoxide na kusababisha yeye na familia yake kupata kizunguzungu.
Watoto wao walianza kuugua kwa haraka huku wakianza kuhisi harufu kali sana ikijaa
Lorelei alieleza: "Hofu kidogo. Asante kwa jumbe zenu na matamshi mema, tuko sawa, asante Mungu."
Aliongeza;"Tuliwasha hita ya maji na hata hivyo hakukuwa na upenyu wa gesi kuondoka hivo kusababisha sumu kali ambayo ilipenya hadi kwa mishipa zetu.
"Nilikuwa nikifanya mazoezi na Jedi na baba yangu, chini. Muda ulipita na nilikuwa na kizunguzungu sana, lakini nilidhani ni mwinuko. Jedi alipanda na baba yangu hadi juu, ambapo wasichana walikuwa na mama yangu.
"Nilimchukua [Jedi] na kuketi kwenye chumba cha wasichana. Jedi alipitiwa na usingizi, niliona ni ajabu sana, na mimi nilianza kusinzia na kulala.
“Mwanamke anayetusaidia kwa nyumba alianza kupiga kelele na kutuambia tutoke nje haraka.
“Tulitoka nje kwa sababu harufu ilikuwa haivumiliki. Annette alikuwa akilia kwa sababu alihisi mgonjwa, Jedi alikuwa amelala na mimi nilikuwa nikiona ulimwengu juu chini.”
Lorelei pia alifichua jinsi yeye na watoto wake walianza kutapika na kuumwa na kichwa huku babake akijaribu kuzima hita.
Pia aliwashukuru wafanyikazi wa matibabu kwa matibabu waliyopokea.
Hata hivyo ,nyota huyo wa zamani wa Manchester United na Chelsea alisema:
"Jana katika familia yangu tulipatwa na tukio lisilotarajiwa ambalo mke wangu, wakwe zangu na watoto wangu 5 walilazwa hospitalini.
“Kutokana na hali hiyo haiwezekani niisindikize timu kwenye mechi tunayotakiwa kukutana nayo katika jiji la Valledupar, nawatakia kila la kheri wachezaji wenzangu, mashabiki wote na wananchi wa Valledupar
"Pia ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa kliniki ya Marly de Chía kwa huduma bora ambayo familia yangu ilipokea wakati wa kukaa katika kliniki yao.
"Asante nyote kwa kuelewa na kwa ujumbe wa msaada!"