Aliyekuwa meneja wa Leicester Craig Shakespeare afariki, 60

Kifo cha Shakespeare kilijiri baada ya mapambano makali na ugonjwa wa saratani

Muhtasari

•Kifo cha Shakespeare kilijiri baada ya mapambano makali na ugonjwa wa saratani uliotambuliwa mnamo Oktoba mwaka jana.

•Shakespeare anakumbukwa mno katika kandanda hasa msimu wake na Leicester wa 2015/2016 ambapo Leicester walitawazwa mabingwa wa kombe la Uingereza.

Aliyekuwa Kocha wa zamani wa Leicester
Image: HISANI

Aliyekuwa meneja wa zamani wa klabu ya Leicester City na nyota wa kusherehekewa wa kandanda, Craig Shakespeare amepiga dunia teke akiwa na  miaka sitini.

Familia ilithibitisha taarifa ya kifo chake mnamo Agosti 2, 2024.

Kifo cha Shakespeare kilijiri baada ya mapambano makali na ugonjwa wa saratani uliotambuliwa mnamo Oktoba mwaka jana.

Shakespeare anakumbukwa mno katika kandanda hasa msimu wake na Leicester wa 2015/2016 ambapo Leicester walitawazwa mabingwa wa kombe la Uingereza.

Shakespeare aliwashangaza wengi baada ya kushinda taji hilo ambalo wengi hawakuwa wanaamini timu kama hiyo ingenyakua kwa urahisi na kupiku timu nyinginezo.

Shakespeare alipigwa kalamu mnamo Oktoba 2017 kufuatia msimu 2017/2018 uliokuwa na changamoto chungu nzima kwenye timu yake ya Leicester.

Hata hivyo, kazi yake ya ukocha haikuishia hapo kwani aliendelea na kazi hiyo hiyo huku akiwa na majukumu mbadala katika kandanda huku akifanya kama kocha msaidizi katika klabu za: Everton, Watford, Aston Villa na Norwich City.

Shakespeare alirudi Leicester kama kocha msaidizi chini ya uongozi wa Dean Smith mnamo Aprili 2023.

Mbali na hayo, anakumbukwa kwa kuwa na mtazamo wa kimbinu vilevile kujitolea kwake kwenye spoti ya kandanda.

Mchango wake katika timu ya Leicester na soka ya Uingereza unabakia kuwa azizi hasa kwenye mchezo ambao mashabiki, wenzake na wachezaji wanatambua.

Ama kweli kifo chake ni pigo kubwa kwa wapenzi wa soka ulimwenguni.