Fahamu kwa nini Arteta aliwaajiri kazi wahuni kuwaibia wachezaji wake wakati wa dinner

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Wazo lilikuwa kufundisha kikosi chake umuhimu wa kuwa tayari, macho na kujiandaa - wakati wote.

Muhtasari

• Mwisho wa chakula, Arteta alisimama na kuwataka timu kuangalia mifuko yao. Wachezaji kadhaa walikosa vitu vya thamani.

Mikel Arteta
Mikel Arteta
Image: Hisani

Jarida la The Atletic FC chini ya mwavuli wa New York Times linaripoti kwamba kocha wa Arsenal alieaajiri wezi kuwaibia wachezaji wake.

Kwa mujibu wa jarida hilo, Arteta alipanga njama hii na wahuni kuwaibia wachezaji wake baadhi ya vitu vyao muhimu wakati wa kikao cha pamoja kwenye chakula cha alasiri.

"Katika chakula cha jioni na wachezaji wake, meneja wa Arsenal Mikel Arteta aliajiri kwa siri timu ya wanyakuzi wataalamu. Wanyakuzi hao wajanja walipewa jukumu la kuzunguka meza, kuchukua simu na pochi kutoka kwa kikosi cha kwanza bila wao kujua," ripoti hiyo ilisema.

Mwisho wa chakula, Arteta alisimama na kuwataka timu kuangalia mifuko yao. Wachezaji kadhaa walikosa vitu vya thamani.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Wazo lilikuwa kufundisha kikosi chake umuhimu wa kuwa tayari, macho na kujiandaa - wakati wote.

Aina hii ya fikra bunifu ni mfano wa Arteta, ambaye huona kila tukio kama fursa ya kujifunza na kujiendeleza.

Ushawishi wake unaonekana katika kila nyanja ya Arsenal.

Wamekuwa timu iliyojengwa kulingana na uainishaji wake, na kilabu kilichoundwa kuzunguka roho yake ya ushindani.

Tamaa yake ya uboreshaji imekuwa ya kuambukiza. Ni mawazo ambayo yameenea katika klabu nzima.

Meneja wa Arsenal anajiandaa kuchukua mikoba ya msimu wake wa tano kamili akiwa na Arsenal.

Mabadiliko tangu achukue madaraka mwaka wa 2019 yamekuwa makubwa. Ingawa Arsenal inachukua mtazamo wa kushirikiana kwa uongozi, hakuna mtu mmoja ambaye amekuwa na athari zaidi kuliko Arteta.