logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gallagher aiaga Chelsea, klabu yake ya tangu utotoni kwa hisia nzito na kuhamia Atletico

Gallagher amekuwa Chelsea tangu akiwa na umri wa miaka 5.

image
na Davis Ojiambo

Michezo21 August 2024 - 11:24

Muhtasari


  • • “Kwa kila mtu katika Chelsea, asante kwa kutimiza ndoto zangu. Imekuwa heshima kubwa kila nilipovaa shati, na ilikuwa ndoto kutimia kuwa nahodha wa timu mara nyingi. Nilipenda kila dakika.”
CONOR GALLAGHER

Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza, Conor Gallagher ameiaga klabu yake ya ujanani, Chelsea kwa ujumbe wenye hisia nzito, saa chache baada ya kuthibitisha kufaulu kwa uhamisho wake kwenda Atletico Madrid ya Uhispania.

Kupitia Instagram, Gallagher ambaye uhamisho wake kwenda Madrid umekumbwa na changamoto si haba kwa wiki kadhaa zilizopita alichapisha video za tangu akiweka saini mkataba wake wa kwanza kwenye klabu ya vijana ya Chelsea.

Aliwashukuru mashabiki wote kwa kumuaminia kwa muda wa miaka 18 ambayo amehudumia klabu hiyo na kupanda ngazi kutoka timu ya vijana wa miaka 8 hadi kuchezea timu ya wakubwa na hata kuwa nahodha msimu uliopita.

“Kwa kila mtu katika Chelsea, asante kwa kutimiza ndoto zangu. Imekuwa heshima kubwa kila nilipovaa shati, na ilikuwa ndoto kutimia kuwa nahodha wa timu mara nyingi. Nilipenda kila dakika.”

“Kumbukumbu hizi zitadumu milele. Nashukuru upendo na support zote kutoka kwa mashabiki. Kusikia wimbo wa jina langu kwenye Bridge ni hisia maalum, na bendera uliyoonyesha ilimaanisha ulimwengu kwangu. Asante kwa kila kitu. Naitakia kilabu kila la heri kwa siku zijazo, na ninatumai kuwaona nyote hivi karibuni huko Stamford Bridge!” Gallagher aliandika kwa hisia.

Mchezaji huyo anahamia Atletico Madrid kwa kitita cha zaidi ya pauni 40.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved