Droo ya robo fainali ya Kombe la Carabao msimu wa 2024–25 ilifanyika siku ya Jumatano usiku huku timu nane pekee zikiwa zimesalia kwenye kinyang'anyiro hicho zikichuana kuwania tuzo hizo.
Southampton na Brentford walijinyakulia tikiti yao ya kutinga hatua ya nane bora wakiwashinda Stoke City na Sheffield Wednesday mtawalia.
Arsenal, Liverpool na Manchester United zilifuzu pia huku Crystal Palace na Newcastle United wakipata ushindi mkubwa dhidi ya Aston Villa na Chelsea mtawalia.
Katika mchuano mkubwa zaidi wa hatua ya 16 bora, Tottenham Hotspur waliwashinda Manchester City nyumbani huku Ange Postecoglou akitafuta taji lake la kwanza kama mkufunzi wa Spurs.
Baada ya kukamilika kwa michuano ya raundi ya 16, ratiba ya robo fainali ilipangwa huku michuano minne ikitarajiwa kuchezwa mnamo Disemba 17, 2024.
Hii ndio orodha kamili ya mechi za robo fainali:
· Tottenham Hotspur dhidi ya Manchester United
· Arsenal dhidi ya Crystal Palace
· Newcastle dhidi ya Brentford
· Southampton dhidi ya Liverpool