Nahodha wa timu ya wasichana ya taifa wasiozidi umri wa miaka 17 Elizabeth Ochaka, amejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 21 cha wachezaji wa timu ya taifa ya wanawake Harambee Starlets kitakachoelekea nchini Morocco kushiriki mechi ya kirafiki kati ya Harambee Starlets na Morocco. Mechi hiyo imeratibiwa kuchezwa Ijumaa Novemba 29 mkondo wa kwanza nchini Morocco na baadaye mechi ya mkondo wa pili kuchezwa nchini humo Jumanne Desemba 3.
Mechi zote mbili zitagaragazwa katika uwanja wa Mohammed VI Football Complex mwendo wa saa mbili usiku majira ya Afrika mashariki.
Kocha wa Harambee Starlets Beldine Odemba ametaja kikosi cha wachezaji 21 watakaosafiri kuelekea Morocco kwa ajili ya mechi hiyo ya kirafiki akiwemo Elizabeth Ochaka.
Beldine ambaye pia ni kocha wa Kenya Police kikaimuC, ametaja kikosi kinachojumuisha magolikipa Annedy Kundu, Christine Adhiambo na Lilian Awuor.
Kwenye safu ya ulinzi na kati. wachezaji Ruth Ingosi, Elizabeth Ochaka, Norah
Ann, Vivian Nasaka, Wincate Kaari, Mango Enez, Christine Adhiambo, Corazone
Aquino, Akinyi Lavender Ann, Fasila Adhiambo na Nyabuto Lorna Nyarinda.
Vile vile, safu ya ushambulizi kikosi alichoteua
Odemba ni Mwanahalima Adam, Beverlyne Adika, Elizabeth Mideva, Violet Nanjala,
Diana Cherono, Elizabeth Mutukiza na Jacklyne Chesang