logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Liverpool kuvaana na Real Madrid Jumatano usiku, klabu bingwa barani Ulaya

Katika mechi 11 za klabu bingwa barani Ulaya baina ya timu hizo mbili Real imeshinda saba na Liverpool kushinda tatu

image
na Brandon Asiema

Football27 November 2024 - 10:10

Muhtasari


  • Timu hizo mbili zimekutana mara tatu katika fainali ya klabu bingwa barani Ulaya Liverpool ikishinda mara moja mwaka wa 1981.
  • Liverpool na Real Madrid walikutana katika hatua ya kumi na sita bora msimu jana mechi ambazo Real Madrid ilishinda mikondo yote miwili kwa jumla ya mabao 6 kwa 2.


Mechi za kombe la klabu bingwa barani Ulaya raundi ya sita zitaendelea kuchezwa Jumatano usiku, jumla ya mechi tisa, zikiratibiwa kuchezwa katika viwanja tofauti tofauti.

Katika ratiba ya leo, wawakilishi wa ligi ya Uingereza Aston Villa na Liverpool watakuwa na vibarua katika viwanja vyao vya nyumbani watakapowaalika Juventus na Real Madrid mtawalia mwendo wa saa tano usiku majira ya Afrika ya mashariki.

Liverpool wanalenga kurudi kileleta kwenye msimamo wa jedwali la klabu bingwa barani Ulaya baada ya mechi ya leo, dhidi ya Real Madrid ambao wanashikilia nafasi ya 21 baada ya mechi nne kwa jumla ya alama sita, alama 6 nyuma ya Liverpool walio katika nafasi ya 3 baada ya mechi nne.

Katika mechi 11 za awali baina ya timu hizo mbili, Real Madrid imeshinda mechi saba huku Liverpool ikifanikiwa kushinda mechi tatu pekee. Timu hizo mbili zilipatana msimu jana kwenye ligi hiyo katika hatua ya kumi na sita bora, ambapo Liverpool kwenye mechi ya mkondo wa kwanza, ilipigwa mabao 5 kwa 2 na Real Madrid huku mkondo wa pili ugani Santiago Bernabeu Real walishinda kwa bao moja.

Aidha timu hizo mbili zimekutana mara tatu kwenye fainali ya UEFA Champions Leage, Liverpool ikishinda mara ya kwanza kwa bao moja mnamo msimu wa 1980/1981. Fainali ya hivi karibuni baina ya timu hizo mbili ilikuwa msimu wa 2021/2022 ambapo Real Madrid iliinyamazisha Liverpool kwa bao moja pekee. Fainali nyingine iliishia kwa ushindinwa mabao 3kwa 1 kwa faida ya Real Madrid katika msimu wa 2017/2018.

Kwenye ratiba nyingine kweny mechi za Jumatano, ni kuwa

·       Crvena Zvezda V VfB Stuttgart   2:45 usiku

·       SK Sturm Graz  V  Girona   2:45 usiku

·       Aston Villa V Juventus  5:00 usiku

·       Monaco  V  Benfica  5:00 usiku

·       PSV   V   Shakhtar Donetsk   5:oo usiku

·       Liverpool  V  Real Madrid  5:00 usiku

·       Celtic   V  Club Brugge  5:00 usiku

·       Bologna  V  LOSC   5;00 usiku

·       Dinamo Zagreb  V  Dortmund  5:00 usiku



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved