Mwanasoka wa Brazil Neymar Junior ametangaza kuwa kombe la dunia la 2026 litakuwa la mwisho kwake kushiriki.
Mshambuliaji huyo wa timu inayoshiriki Saudi Pro League ya Al Hilal amekuwa akikabiliwa na majeraha ya kila mara, Kabla ya kushiriki kombe la dunia, Neymar lazima apone kikamilifu.
Mnamo Oktoba 2023, alipata jeraha baya la goti wakati wa mechi ya kufuzu dhidi ya Uruguay, ambayo iliisha kwa Brazil kuchapwa 2-0.
Tangu wakati huo, Neymar hajaonekana akiichezea timu ya taifa ya Brazil huku katika klabu yake ya Al-Hilal amecheza mechi mbili pekee tangu kupona jeraha hilo.
Katika mahojiano yake na runinga ya CNN Neymar alisema kwamba ana imani kuwa timu yake ya laifa litafuzu katika michuano za fainali za Amerika Kaskazini.
"Najua hili litakuwa Kombe langu la mwisho la Dunia, shuti langu la mwisho, nafasi yangu ya mwisho na nitafanya kila niwezalo kucheza ndani yake," Aliiambia CNN.
Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 32, ambaye hajaichezea Brazil kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa kutokana na jeraha vile vile alikiri kuwa hana ubaya iwapo atapata nafasi ya kujiunga na timu ya Inter Miami ambapo iwapo atajiunga nao atapata nafasi ya kuungana tena na wachezaji wenzake wa zamani wa Barcelona kama vile Lionel Messi na Luis Suarez.
Brazil imeonekana kutatizika katika kufuzu kwa kombe la dunia la awamu ijayo litakalofanyika katika mataifa matatu ya bara ya Amerika Kusini, Nchi hizao ni Mexico, Marekani na Canada.
Baada ya raundi 12 kati ya 18, wanashika nafasi ya tano katika kundi la mataifa 10. Lakini sita bora wamehakikishiwa nafasi katika Kombe la Dunia na Brazil wako pointi tano mbele ya Bolivia ambao wako katika nafasi ya saba.
Neymar aliwakilisha nchi yake ya Brazil kwenye kombe la dunia la 2014, 2018 na 2022, lakini bado hajabahatika kushinda kombe hilo. Neymar alidokeza kuwa alimwona mchezaji mwenza wa PSG Messi akishinda kombe hilo wakati wa kombe la dunia nchini Qatar na mafanikio ya Argentina yakithibitisha kwamba uvumilivu unaweza kuzawadiwa.
“Messi daima amekuwa msukumo. Sikuzote alinisaidia na kunitia moyo. Ni wazi, kumuona akishinda akiwa na miaka 35, mimi hufikiria kulihusu pia,’’ Alisema Neymar.
Kombe la Dunia lililotanuliwa litashirikisha timu 48 hii ikiwa ni timu 16 zaidi ya Qatar 2022. Fainali ya ngarambe hiyo itagaragazwa Marekani mwaka wa 2026.