logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kipa wa Barcelona Ter Stegen na mkewe Daniela watangaza kuvunjika kwa ndoa yao ya miaka 8

Stegen ametangaza rasmi kutengana na mkewe, Daniela Jehle, baada ya ndoa yao kudumu kwa miaka minane.

image
na Samuel Mainajournalist

Football07 March 2025 - 12:04

Muhtasari


  • Ter Stegen alieleza kuwa yeye na Daniela wamefanya uamuzi huo kwa umakini mkubwa.
  • Daniela alieleza kwamba uamuzi huo ulitokana na changamoto za ndoa.

Kipa Marc -Andre ter Stegen na Daniela Jehle

Mlinda lango wa klabu ya FC Barcelona na timu ya taifa ya Ujerumani, Marc-André ter Stegen, ametangaza rasmi kutengana na mkewe, Daniela Jehle, baada ya ndoa yao kudumu kwa miaka minane.

Kupitia taarifa aliyoichapisha kwenye mitandao ya kijamii, Ter Stegen alieleza kuwa yeye na Daniela wamefanya uamuzi huo kwa umakini mkubwa.

"Baada ya tafakari ya muda mrefu, tumeamua kutengana kwa amani. Hili halikuwa jambo rahisi, lakini ni uamuzi tulioufanya kwa manufaa ya kila mmoja wetu," alisema Ter Stegen siku ya Alhamisi.

Mwanasoka huyo aliongeza kuwa licha ya kutengana, wao wataendelea kushirikiana kama wazazi wa watoto wao wawili.

"Watoto wetu ndiyo jambo la muhimu zaidi kwetu. Tutahakikisha wanakua katika mazingira yenye upendo na utulivu," aliandika.

Kwa upande wake, Daniela Jehle pia alitoa tamko lake kupitia Instagram akieleza kwamba uamuzi huo ulitokana na changamoto za ndoa.

"Hatukufanya uamuzi huu kwa wepesi. Tumepitia changamoto nyingi kama wanandoa, na mwishowe tumeona kuwa njia bora ni kila mmoja wetu kuchukua mkondo wake," aliandika.

Taarifa ya wawili hao imezua maoni mseto miongoni mwa mashabiki wa soka.

"Huu ni mshtuko mkubwa. Walionekana kuwa na ndoa imara," aliandika shabiki mmoja kwenye X (zamani Twitter).

Tangazo hili linakuja wakati ambapo Ter Stegen anapambana kurejea uwanjani baada ya jeraha la goti alilopata mnamo Septemba 2024.

"Nimekuwa nikijitahidi kurudi kwenye kiwango changu bora. Nitaendelea kupambana ndani na nje ya uwanja," alisema kipa huyo wa Barcelona.

Huku maisha yake binafsi yakipitia mabadiliko makubwa, Ter Stegen anaendelea na maandalizi ya kurejea uwanjani, huku mashabiki wake wakimtumia jumbe za faraja na kumtakia kila la heri.


Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved