
Nyota wa zamani wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Wayne Rooney, amejipata katika hali ya aibu baada ya kunaswa kwenye kamera akijisaidia ukutani wakati wa usiku wa starehe jijini London.
Rooney, mwenye umri wa miaka 39, alikuwa ameenda kujiburudisha na marafiki zake katika maeneo ya Marylebone na Mayfair, ambapo walifurahia muda wao katika baa ya kifahari ya The Nest rooftop bar siku ya Jumamosi kabla ya kuhamia kwenye mgahawa wa kifahari wa Novikov.
Iliripotiwa kuwa waliondoka kwenye eneo hilo mwendo wa saa nane usiku kabla ya Rooney kuonekana akijisaidia hadharani.
Akiwa amevalia suti rasmi yenye rangi nyeusi, shati jeupe na tai, Rooney alivuka barabara akiwa na simu mkononi na kisha kuamua kujisaidia ukutani mbele ya wapita njia, huku mwanga wa simu yake ukimulika uso wake. Baada ya kumaliza shughuli hiyo, alirejea kwa marafiki zake akiwa na tabasamu.
Tukio hili si mara ya kwanza kwa Rooney kupatikana akikojoa hadharani. Mnamo mwaka wa 2013, alinaswa akijisaidia dhidi ya pipa jijini Manchester, na kumekuwa na visa vingine vya awali ambapo amepigwa picha akifanya jambo hilo karibu na vichaka.
Ingawa hakuna malalamiko rasmi yaliyoripotiwa kwa polisi wa Metropolitan kuhusu tukio hili, sheria za Westminster zinaweza kumfanya Rooney akabiliwe na faini ya pauni 150 ikiwa angekamatwa na maafisa wa usalama.
Sheria kama vile Public Order Act 1986 na Environmental Protection Act 1990 zinaweza kutumika kwa tabia kama hiyo kulingana na mazingira ya tukio.
Jiji la London, hasa eneo la Soho, liliweka ‘rangi maalum ya kuzuia mkojo’ mnamo mwaka wa 2023 ili kupunguza tabia ya watu kukojoa hadharani. Rangi hiyo maalum hurudisha mkojo kwa mkojoaji kama hatua ya kumzuia kurudia kitendo hicho. Baraza la Westminster lilifichua kuwa gharama ya kusafisha mkojo mitaani ilikuwa inakaribia pauni 950,000 kwa mwaka.
Baada ya tukio hilo, Rooney alionekana kwenye televisheni kama mchambuzi wa mpira wa miguu kwenye BBC wakati wa mechi ya robo fainali ya Kombe la FA kati ya Brighton na Nottingham Forest.
Hata hivyo, licha ya kutoa maoni yake makali kuhusu uteuzi wa kikosi cha Nottingham Forest, timu hiyo ilishinda mechi hiyo kupitia mikwaju ya penalti.
Tukio la Rooney limezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii, huku wengi wakijiuliza kama tabia yake inahusiana na utamaduni wa ulevi wa wanasoka wa zamani au ni jambo la kawaida kwake