AFCON 2023: Tazama matokeo ya Jumatano, Ratiba ya michuano ya Alhamisi

Mechi mbili za kusisimua zikichezwa kwa nyakati tofauti katika uwanja wa Stade Laurent Pokou mnamo Jumatano usiku.

Muhtasari

•Simba Stars ya Tanzania ilimenyana na wababe wa sasa wa Afrika, Morocco ambao waliwazaba mabao 3-0 na kuwaacha wa mwisho katika kundi F.

•D.R Congo na Zambia na iliisha kwa sare ya 1-1 baada ya timu zote mbili kumenyana kishujaa kwa dakika zote 90.

iliwalima Tanzania mabao 3-0 mnamo Jumatano jioni.
Morocco iliwalima Tanzania mabao 3-0 mnamo Jumatano jioni.
Image: FACEBOOK// AFCON

Michuano inayoendelea ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2023) iliingia siku ya tano Jumatano jioni huku timu zote kwenye mashindano hayo sasa zikiwa zimecheza mechi moja kila moja.

Siku ya tano ya mashindano ya Afrika mwaka huu ilishuhudia mechi mbili za kusisimua zikichezwa kwa nyakati tofauti katika uwanja wa Stade Laurent Pokou mjini San Pedro, Ivory Coast.

Katika mechi ya kwanza ya Jumatano jioni, Simba Stars ya Tanzania ilimenyana na wababe wa sasa wa Afrika, Morocco ambao waliwazaba mabao 3-0 na kuwaacha wa mwisho katika kundi F.

Nahodha wa Morocco, Roman Saiss alianza kufunga katika dakika ya 30 kabla ya kiungo Azzedine Ounahi na mshambuliaji Youssef En Nesyri kuongeza mabao mengine mawili katika kipindi cha pili.

Tanzania ililazimika kukamilisha mechi hiyo ikiwa na wachezaji 10 pekee uwanjani baada ya beki Novatus Miroshi kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 70.

Mechi ya mwisho jioni ilikuwa kati ya D.R Congo na Zambia na iliisha kwa sare ya 1-1 baada ya timu zote mbili kumenyana kishujaa kwa dakika zote 90.

Zambia walianza kufunga katika dakika ya 23 kupitia kwa kiungo Kings Kangwa kabla ya mshambuliaji Yoanne Wissa wa Brentford kuisawazishia DRC Kongo takriban dakika nne baadaye. Hakuna mabao zaidi yaliyofungwa katika kipindi cha pili.

Timu zote sasa zitaanza kucheza mechi zao za pili za michuano ya AFCON 2023 Alhamisi jioni wakati mechi tatu tofauti zinatarajiwa kuchezwa.

Tazama ratiba ya mechi za Alhamisi, Januari 18;-

Equatorial Guinea vs Guinea Bissau (Saa kumi na jioni moja masaa ya Afrika Mashariki katika uwanja wa Stade Olympique Allasane Quattara)

Ivory Coast vs Nigeria (Saa mbili usiku masaa ya Afrika Mashariki katika uwanja wa Stade Olympique Allasane Quattara)

Egypt vs Ghana (Saa tano usiku masaa ya Afrika Mashariki katika uwanja wa Stade Felix Houphoet-Boigny, Abijan)