logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Benjamin Mendy arejelea soka baada ya kuondolewa mashtaka ya ubakaji, asainiwa Ufaransa

FC Lorient imemtangaza beki wa zamani wa Manchester City Benjamin Mendy kama mchezaji wao mpya.

image
na Radio Jambo

Makala19 July 2023 - 09:45

Muhtasari


•FC Lorient imetangaza kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amesaini nao mkataba wa miaka miwili..

•Klabu hiyo ilifichua kuwa Mendy atavaa jezi namba 5 na ataanza mazoezi yake ya awali hivi leo, Jumatano.

Klabu ya Ligue 1,  FC Lorient imemtangaza beki wa zamani wa Manchester City Benjamin Mendy kama mchezaji wao mpya.

Katika taarifa ya siku ya Jumatano adhuhuri, klabu hiyo ya Ufaransa ilitangaza kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amesaini nao mkataba wa miaka miwili..

"FC Lorient inafuraha kutangaza leo usajili wa beki wa kushoto wa kimataifa wa Ufaransa Benjamin Mendy (29) kwa misimu miwili," taarifa iliyoshirikiwa kwenye tovuti rasmi ya Lorient ilisoma.

"Baada ya kuridhika na uchunguzi wa kiafya, Benjamin Mendy, bingwa wa dunia wa 2018, mshindi mara nne wa Ligi ya Premia chini ya klabu ya Manchester City na bingwa wa Ufaransa wa Ligue 1 akiwa na Monaco haswa, anakuja kuimarisha nguvu kazi ya Lorient kwa msimu huu mpya, ” taarifa hiyo ilisomeka.

Klabu hiyo ilifichua kuwa Mendy atavaa jezi namba 5 na ataanza mazoezi yake ya awali hivi leo, Jumatano huku akijiandaa kucheza msimu ujao.

Haya yanajiri siku chache tu baada ya mahakama kutangaza kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 hana hatia baada ya kumuondolewa mashtaka yote ya ubakaji dhidi yake. Mendy hajacheza kwa zaidi ya miaka miwili tangu alipokamatwa na kushtakiwa kwa tuhuma za ubakaji mnamo Novemba 2020.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved