logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mikel Arteta ashutumiwa kwa kumdhalilisha marehemu mamake kocha wa Porto wakati wa mechi

"Arteta aligeukia benchi wakati wa mchezo na kuitukana familia yangu kwa Kihispania," Kocha Sergio alidai.

image
na Samuel Maina

Michezo14 March 2024 - 05:06

Muhtasari


  • •Mwishoni mwa mechi, Kocha Sergio alionekana akimlalamikia Arteta kwa hasira kwa kile ambacho mashabiki hawakuweza kufahamu.
  • •"Arteta aligeukia benchi wakati wa mchezo na kuitukana familia yangu kwa Kihispania," Kocha Sergio alidai.
Mikel Arteta

Meneja wa Porto Sergio Conceicao aliibua madai mazito dhidi ya mwenzake wa Arsenal Mikel Arteta Jumanne usiku kufuatia mechi yao ya kusisimua kwenye uwanja wa Emirates.

Wanabunduki waliwashinda Porto 4-2 kwa mikwaju ya penalti baada ya mechi kali ya hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyoisha 1-0 katika dakika 90 za kawaida pamoja na dakika 30 za ziada, matokeo yaliyowasaidia kufuzu kwa robo fainali ya shindano hilo. Mwishoni mwa mechi hiyo, Kocha Sergio alionekana akimlalamikia Arteta kwa hasira kwa kile ambacho mashabiki hawakuweza kufahamu.

Huku akizungumza na wanahabari baada ya mechi hiyo, Mreno huyo alidai kuwa kocha huyo wa Arsenal aliitukana familia yake kwa lugha ya Kihispaniola.

"Arteta aligeukia benchi wakati wa mchezo na kuitukana familia yangu kwa Kihispania," Kocha Sergio alidai.

Aliongeza, “Nilimwambia huyo aliyemtukana hayupo tena miongoni mwetu. Mwacheni ahangaike kuifundisha timu yake ambayo ina ubora zaidi ya kucheza vizuri zaidi.

Makocha hao wawili ambao wote walipata kadi nyekundu wakati wa mchezo huo walionekana wakishiriki mazungumzo makali baada ya mikwaju ya penalti iliyoifanya Arsenal kushinda.

Wakati akijibu madai yaliyotolewa na mpinzani wake wa usiku huo, Mikel Arteta alionekana kususia kutoa maoni yoyote kuhusu hilo.

"Sina la kusema. Asante sana,” Arteta alimwambia mwandishi wa habari alipotakiwa kujibu.

Vyanzo vya habari kutoka klabu ya soka ya Arsenal hata hivyo vimekanusha madai yoyote ya matusi au matusi dhidi ya meneja wa Porto.

Jumanne usiku, Wanabunduki walifuzu kwa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza baada ya takriban miaka 14. Mara ya mwisho walifanikiwa kutoka katika hatua ya makundi mwaka 2010.

Mshambulizi Leandro Trossard alifungia washika bunduki katika kipindi cha kwanza cha mechi ya Jumanne na kufanya jumla ya matokeo kuwa 1-1. Vijana wa Mikel Arteta walikuwa wamepoteza kwa Porto 1-0 wakati wa mechi ya mkondo wa kwanza iliyochezwa Ureno wiki chache zilizopita.

Nahodha Martin Odegaard, Bukayo Saka, Kai Havertz na Declan Rice kisha wakafungia klabu hiyo penalti huku kipa David Raya akiokoa penalti mbili.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved