SHIDA YA BIPOLAR

Ombachi afunguka kuhusu vita vyake dhidi ya 'Bi-polar'

“Miaka mingi nimepambana na hali hii pamoja na huzuni. Ningepotea mitandao ghafla na kwa saa zingine nakosa kuabiri ndege hata nikiwa nishahitimu kuwa kwenye timu ya taifa” Ombachi alieleza.

Muhtasari

• Alisema kuwa shida hiyo ilimfanya alaumiwe sana kwa nyakati kama zile za kukosa ndege ama kupata shida yoyote na timu.

•Alisema kuwa wanariadha wengi wanapitia shida hii na wanahitaji usaidizi wenu na kueleweka.

Dennis Ombachi
Dennis Ombachi
Image: Instagram

Mcheza raga wa Kenya 7s Dennis Ombachi amefunguka kuhusu vita yake na shida ya ‘Bipolar’

Kupitia ujumbe katika mtandao wa Twitter, Ombachi amekiri kuwa uchunguzi wa daktari ulidhibitisha kuwa yeye ni mwathiriwa wa ashida hiyoya kupata vipindi za huzuni kubwa mara kwa mara ikibadilishana na vipindi vya raha kubwa mara zingine.

Miaka mingi nimepambana na hali hii pamoja na huzuni. Ningepotea mitandao ghafla na kwa  saa zingine nakosa kuabiri ndege hata nikiwa nishahitimu kuwa kwenye timu ya taifa” Ombachi alieleza.

Mchezaji huyo ambaye pia ni mpishi mkuu alisema kuwa shida hiyo ilimfanya alaumiwe sana kwa nyakati kama zile za kukosa ndege ama kupata shida yoyote na timu.

Walisema  ‘nakuwa Dennis tu’, kile ambacho kocha na wachezaji wenzangu hawakujua ni kuwa nilikuwa na machungu sana” alieleza Ombachi.

Alieleza kuwa familia yake imemsaidia sana kupambana na hali hiyo huku akisema madawa apatayo humsaidia kutulia.

Wanariadha wengi wanapitia shida hii na wanahitaji usaidizi wenu na kueleweka. Tukizungumzia jambo hili basi watu hawataumia kwa kimya kama nilivyoumia mimi” alikiri Ombachi.

Aliagiza Wakenya kuzungumzia shida hiyo na kusaidia wanaipitia kwani wanahitaji usaidizi mkubwa.