Naibu Rais William Ruto ameghairi mikutano yote ya Kenya Kwanza Alliance kwa muda wa siku tatu zijazo.
Kusimamishwa huko kunafuatia kifo cha aliyekuwa Rais Mwai Kibaki.
Katibu wa Dijitali wa Ruto Dennis Itumbi kupitia kwenye mtandao wake a twitter alitangaza habari za kusimamishwa kwa kampeni hizo.
Muungano ulikuwa umepanga ziara ya siku nne ya kampeni katika Kaunti ya Vihiga, iliyohusisha Bungoma, Busia na Kakamega hadi Jumapili, Aprili 24.
Hapo awali, Naibu Rais alisema marehemu Kibaki alikuwa msukumo mkubwa kwa Muungano wa Kenya Kwanza kwa umakini wake wa kiuchumi.
Urais wa Kibaki uliegemezwa kufufua uchumi wa nchi baada ya miaka mingi ya kudorora.
Katika wakati wake, Kibaki alipanua wigo wa mapato na ukusanyaji wa Kenya, na alifanya kazi ili kulipia nchi deni.
Ruto alikuwa akizungumza wakati wa kongamano la Kiuchumi la Kaunti ya Kakamega lililofanyika katika Shule ya Upili ya Musingu.
Muungano ulitarajiwa kuwa na mkutano Butula, Luanda na Eshisiru siku ya Ijumaa.