Mwaniaji wa kiti cha ugavana Nairobi Agnes Kagure amekariri kwamba bado yuko kwenye kinyang'anyiro cha kuwania kiti cha ugavana Nairobi, licha ya ripoti kudokeza kuwa ameachana na azma yake ya kumpendelea Polycarp Igathe.
Kupitia mtandao wa Facebook, Kagure alitaja ripoti hizo kuwa tetesi huku akisisitiza kwamba bado yuko kwenye kinyang'anyiro cha kunyakua kiti cha juu cha City Hall, akidokeza kwamba huenda akachukua njia huru.
"Tetesi nyingi sana zinasambazwa na mawakala wa uharibifu, lakini ni uvumi wa bure tu! Safari hii tulianza miaka iliyopita na kuizindua rasmi tarehe 7 Januari. Sina mpango wa kuwaacha mamia ya maelfu wanaoamini katika nusu yake,” alisema.
“Ndoto yetu ya Nairobi bora ambayo inaunga mkono talanta na matamanio yetu, jiji ambalo ni husuda ya miji mingine, na kaunti inayotunza wakaazi wake. kwa uthabiti kwenye njia."
Aliyekuwa Afisa Mkuu wa Equity (CCO) Igathe Alhamisi alisema kwamba Kagure pamoja na Mbunge wa Westlands Tim Wanyonyi na mfanyabiashara Richard Ngatia, walikubali kuacha zabuni zao na kumuunga mkono, kufuatia kile alichokitaja kuwa mazungumzo ya makubaliano yaliyofaulu.
Maoni ya Igathe yalifuatia mjadala wa siku nzima katika Ikulu ya Nairobi, siku ya Alhamisi kuhusu nani kati yake na watatu, wangepeperusha bendera ya Azimio One Kenya katika kinyangpanyiro cha ugavana.