Seneta wa Bungoma Moses Wetangula amesema kuwa rais Uhuru Kenyatta hafai kutumia vibaya mamlaka aliyopewa na Wakenya kwa kukasirikia Mkenya yeyote.
"Tarehe 1,Mei nilimuona Mheshimiwa Rais amesimama na nilimuona kuwa amekasirika sana, ushauri wa bure kwa Rais ni kuwa tumekupa vyombo vyote vya mamlaka hatukukuchagua ili kumkasirikia Mkenya yeyote kwa sababu unaweza kutumia vibaya madaraka yako kirahisi unapomkasirikia Mkenya yeyote". Moses Wetangula alisema.
Seneta huyo ambaye amekuwa katika mstari wa mbele kupigia debe naibu rais William Ruto kuwa rais katika uchaguzi mkuu wa Agosti aliongeza kuwa;
"Tulikuchagua ili uhakikishe kwamba wakenya wanamudu chakula,tulikucagua ili uhakikishe kuna elimu, pia tulikuchagua ili uhakikishe kwamba kil mkenya ana imani na usalama wa kutosha," Alizungumza Wetangula.
Moses Wetangula alisema haya alipokuwa akizungumza katika kaunti ya Kisii huku Kenya Kwanza ikiendelea kueneza mtindo wao wa kiuchumi wa bottom-up katika eneo la Nyanza.
Rais Uhuru Kenyatta hapo awali alimshutumu mkuu wa pili wa jamhuri ya Kenya William Ruto kwa kuacha kazi yake lakini akapendelea kuzunguka nchi nzima akisema uongo kuhusu utawala wake.
Baadhi ya Wakenya pia wameelezea kusikitishwa kwao na jinsi rais Uhuru Kenyatta na naibu rais William Ruto wamekuwa wakionyesha uongozi mbaya.