Baada ya kuondolewa mashtaka ya uchochezi wa ghasia, Mbunge wa Tiaty William Kamket anaelekea katika Mahakama ya Juu kutafuta fidia kwa kile alichodai kuwa ni kukamatwa kwa nia mbaya na kufunguliwa mashtaka.
Mbunge huyo kupitia kwa wakili wake Kipkoech Ngetich, akizungumza na wanahabari, alisema atawasilisha kesi mjini Nakuru kupinga serikali na kupewa fidia ya Sh100 milioni.
Bw Ngetich alisema mteja wake ni Mbunge mashuhuri ambaye alinyanyaswa, aliaibishwa na kufanyiwa mzaha na umma alipohusishwa na mapigano yaliyokumba eneo la Ol Moran Kaunti ya Laikipia.
Alisema polisi walitumia mfumo wa mahakama kumuadhibu mteja wake kupitia mashtaka ya uzushi ambayo hayana ushahidi.
Alieleza kuwa uamuzi wa mahakama wa kumwachilia Bw Kamket ulionyesha kwamba hakuwa na hatia na kwamba polisi walikuwa wakimtumia kukwepa utendakazi wao katika kukabiliana na ghasia katika Bonde la Kerio.
"Mteja wangu ameachiliwa chini ya kifungu cha 210 cha kanuni za utaratibu wa uhalifu, ambayo ina maana kwamba hakukuwa na kesi dhidi yake," Bw Ngetich.
"Tutafungua kesi ya kutaka fidia ya Sh100 milioni na fidia kwa upande wa mashtaka yenye nia mbaya kutoka kwa serikali ili iwe fundisho kwa matendo yao."
Bw Kamket alikamatwa nyumbani kwake katika Kaunti ya Baringo mnamo Septemba 8 kabla ya kuhamishwa hadi Kaunti ya Nakuru. Alizuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Kaptembwo ambako alilala.
Alipofikishwa mahakamani siku iliyofuata, polisi walitaka kumzuilia Bw Kamket kwa wiki mbili, wakidai alishukiwa kuhusika katika kupanga uvamizi wa ardhi na kuwachochea wafugaji haramu kushambulia jamii za Ol Moran.
Bw Kamket alishtakiwa kwa kutoa taarifa za uchochezi mnamo Septemba 10.
Kwa sababu waendesha mashtaka "walikosa kuwaita mashahidi wowote au kutoa ushahidi wowote, kesi dhidi ya mshtakiwa inatupiliwa mbali kwa kukosa kufunguliwa mashtaka na mshtakiwa anaachiliwa huru chini ya Kifungu cha 210 cha kanuni za utaratibu wa uhalifu," Bi Nyaloti aliamua.
Bw Ngetich alikubaliana na uamuzi huo, akisema ulikuwa ushindi mkubwa kwa utawala wa sheria.