logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Raila kususia mdahalo wa urais? mkurugenzi wa mawasiliano kampeni za Raila adokeza

“Mdahalo uliofeli. Kuharibu kwa muda muhimu wa wagombea. Kama huu ndio mdahalo basi msiwe na uhakika sana,” - Dennis Onyango.

image
na Radio Jambo

Habari20 July 2022 - 12:27

Muhtasari


• Watu wengi walikejeli jinsi mdahalo wa wagombea wenza ulivyokuwa bila ladha kaam ambavyo wengi walikuwa wanategemea.

• "Kama huu ndio mdahalo basi msiwe na uhakika sana,” mwandani huyo wa Raila alidokeza.

Mgombea urais Raila Odinga

Dennis Onyango, mwandani wa kinara wa Azimio la Umoja One Kenya, Raila Odinga amedokeza kwamba huenda Raila atakwepa kushiriki katika mdahalo wa wagombea urais unaoratibiwa kufanyika Julai 24, wiki kesho.

Kupitia kwa ukurasa wake wa Twitter, Onyango alikemea na kukejeli jinsi ambavyo mdahalo wa wagombea wenza wa urais ulivyokuwa hauna nguvu na kusema kwamba kama hilo ndilo litafanyika katika mdahalo wa wagombea urais basi wakenya wasiwe na uhakika sana.

Matamshi yake hayo japo hakusema moja kwa moja kwamba Raila atasusia mdahalo huo lakini yalikisia kwa asilimia kubwa kwamba kama mdahalo hafifu kama ule wa wagombea wenza ndio utakuwa wa wagombea urais basi wakenya wasiwe na uhakika sana wa Raila kuhudhuria.

“Mdahalo uliofeli. Kuharibu kwa muda muhimu wa wagombea. Hafifu sana. Unakaa kibiashara na umbea. Panakosekana kabisa ladha. Kama huu ndio mdahalo basi msiwe na uhakika sana,” mwandani huyo wa Raila alidokeza.

Onyango ambaye ni mkurugenzi wa mawasiliano na katibu katika kampeni za Raila Odinga alichukizwa na jinsi mdahalo wa wagombea wenza ulivyokosa ladha na chachu ile iliyokuwa ikitarajiwa na kusema kwamba hata kidogo haukufikia viwango ambavyo wengi walikuwa wanatarajia na kusubiria kwa hamu kubwa.

Ujumbe huo fiche kutoka kwa Onyango uliwachanganya wengi baadhi wakishindwa kuuelewa na wengine wakiutafsiri kwamab alikuwa na maana watu wasitegemee kumuona Raila akishiriki kama viwango vya mdahalo viko chini kwa kiwango kile kilichoonekana kwenye mdahalo wa wagombea wenza.

“Ati hawapaswi kuwa na uhakika sana? Hawapaswi kuwa na uhakika wa Raila kuhudhuria?😂😂Bado bado,” mmoja kwa jina Migosi Brian alitaka kufafanuliwa zaidi.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved