Huku vifaa vya uchaguzi mkuu vikiendelea kusafirishwa katika vituo mbali mbali nchini kwa ajili ya uchaguzi mkuu Kesho, inaarifiwa kwamba gari moja lililokuwa limebeba vifaa hivyo kusambaza katika vituo eneo bunge la Chuka Igambang’ombe vimeharibiwa na wananchi waliokuwa na ghadhabu.
Haya yanajiri chini ya saa 24 kabla ya uchaguzi Mkuu ambapo Wakenya wanatarajiwa kuipigia kura serikali ijayo.
IEBC ilikuwa bado haijatoa taarifa kuhusu tukio hilo kufikia wakati wa Tukio hilo. Tupo ange kutoa majibu yao mara tu watakapofanya.
Picha za vifaa zvlivyoharibiwa vilivyoonekana na kituo hiki vilionyesha karatasi na mihuri ya usalama iliyoenea chini.
Bado haijulikani ni nini kilichochea uharibifu wa nyenzo.
IEBC ilianza usambazaji wa vifaa vya uchaguzi katika vituo vya kupigia kura Jumatatu.
Wapiga kura wanatarajiwa kuanza kupiga kura siku ya Jumanne saa kumi na mbili asubuhi. Zoezi hilo litakamilika saa 5 usiku.
IEBC ilikuwa bado haijatoa taarifa kuhusu tukio hilo kufikia wakati wa kwenda kwa vyombo vya habari. Tunajitolea kutoa majibu yao mara tu watakapofanya.
Hata hivyo, afisa wa IEBC alifahamisha wanahabari akisema kulikuwa na mchanganyiko wa karatasi za kupigia kura katika kaunti hiyo.
Awali kule Tharaka Nithi afisa wa uchaguzi wa IEBC Mohammed Raka alisema kulikuwa na mkanganyiko hapo awali ambapo karatasi za kupigia kura wadi ya Fafi, Kaunti ya Garissa zilipatikana Chuka.
"Kumekuwa na mkanganyiko ambapo karatasi za kupigia kura za wadi ya Fafi zimepatikana Chuka. Tumemjulisha afisa wetu wa Nairobi na wanashughulikia suala hilo," alisema.
Raka alifichua kuwa karatasi sahihi za kura zitaletwa Chuka kwa chopa na zile zinazofaa zitatumwa Garissa.
"Hadi sasa hili ni tukio pekee ambalo limeripotiwa kote nchini na linatatuliwa mara moja," aliongeza.
IEBC ilianza usambazaji wa vifaa vya uchaguzi katika vituo vya kupigia kura Jumatatu.
Wapiga kura wanatarajiwa kuanza kupiga kura siku ya Jumanne saa kumi na mbili asubuhi. Zoezi hilo litakamilika saa 5 usiku.