Mgombea urais wa UDA alipata kura 720 katika eneo la Bondo, eneo bunge la Raila Odinga.
Raila wa Azimio la Umoja One Kenya Coalition Party alipata kura 73,603.
Mgombea urais wa vyama vya Agano Waihiga Mwaure na kinara wa Chama cha Roots George Wajackoya walipata kura 22 na 94 mtawalia.
Haya ni kwa mujibu wa kujumlisha matokeo ya urais yaliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi katika eneo bunge hilo Dennis Omari Obara Jumatano usiku.