logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Ghasia katika kituo cha kuhesabia kura cha Jamhuri baada ya sanduku lenye shaka kuwasilishwa

Pia kulikuwa na suala pia la kuchelewa kutangazwa kwa matokeo jambo ambalo lilizua hofu.

image
na

Habari10 August 2022 - 21:21

Muhtasari


•Vurugu zilizuka baada ya wapiga kura kudai kuwa masanduku hayo mawili ya kura yalikuwa yakiletwa kujumlishwa chini ya hali isiyoeleweka.

•Mtazamaji wa uchaguzi alisema kuwa kuna suala pia la kuchelewa kutangazwa kwa matokeo jambo ambalo lilizua hofu.

Makarani wa IEBC katika kituo cha kuhesabia kura cha Kasarani wakati wa kuwasilisha masanduku ya kura na fomu 37A Jumatano, Agosti 10, 2022.

Ghasia zilizuka katika kituo cha kujumlishia kura cha Jamhuri jijini Nairobi baada ya wapiga kura kusitisha majaribio ya kuleta sanduku la kura lisilotambulishwa.

Vurugu zilizuka baada ya wapiga kura kudai kuwa masanduku hayo mawili ya kura yalikuwa yakiletwa kujumlishwa chini ya hali isiyoeleweka.

"Hatujui masanduku hayo mawili yalitoka wapi na nia ya nani aliyezileta hapa," Mtazamaji wa uchaguzi ilisema.

"Hizo sanduku mbili hatujui zilitoka wapi, ni nani alizileta na nia yao ilikua nini."

Mtazamaji huyo wa uchaguzi alisema kulikuwa na swali kuhusu masanduku hayo mawili ya kura yalitoka wapi baada ya vifaa vingine vya uchaguzi vilivyosalia kuwasilishwa mara baada ya shughuli ya kupiga kura kukamilika.

"Kwa nini imechukua muda mrefu sana kwa masanduku hayo mawili kufika hapa mawili, wakati tunakaribia kumaliza kuhesabu," alihoji.

Aliongeza kuwa kuna suala pia la kuchelewa kutangazwa kwa matokeo jambo ambalo lilizua hofu.

"Kuhesabu kwa matokeo kulifanyika muda mfupi uliopita lakini hadi sasa mshindi hajatangazwa," alisema.

Ucheleweshaji huo uliitwa na mwangalizi kama jaribio la kuchakachua na kudhibiti matokeo.

Wale waliokuwa wakizunguka eneo hilo wakati huo, walibadilishana vikali na maafisa wa polisi waliokuwa wakijaribu kuzuia hali hiyo.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved