logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Muitaliano Aliyewania Ugavana Kilifi Astaafu Siasa Baada ya Kupata Kura 2K, Kupoteza mara 3

“Nadhani nitastaafu baada ya hili, Lakini nitabaki Kenya kwa sababu ni nchi yangu ninayoipenda na nitafia hapa" - Esposito

image
na Davis Ojiambo

Uchaguzi13 August 2022 - 14:33

Muhtasari


  • • Hii ni mara ya tatu Muitaliano huyo anajaribu bahati yake katika karata chafu ya siasa ila mara zote tatu amepoteza.
Mwansiasa Mweney asili ya Italia, Franco Esposito

 Muitaliano mkaazi wa Kenya aliyekuwa anawania ugavana Kilifi, mzee Franco Esposito amedokeza kwamba huenda atastaafu kutoka siasa za Kenya baada ya kushindwa katika chaguzi tatu mtawalia.

Esposito ambaye anamiliki biashara za kifahari katika kaunti ya Kilifi ana asili ya Italia na amekuwa akijaribu karata yake katika siasa kwa mara ya tatu bila mafanikio.

Mwanasiasa huyo alikuwa anawania ugavana kama mgombea huru na alibwaga kwa kupata kura takribani elfu mbili na mia saba tu katika kaunti nzima na jambo hili lilionekana kumuuma sana hadi kusema kwamba huenda akawekeza nguvu na muda mwingi katika biashara zake huko Malindi na kuachana na siasa.

Licha ya kuanguka, Esposito alisema uchaguzi ulikuwa wa amani na kila kitu kilienda vizuri kama kilivyoratibiwa, hata ingawa kulikuwepo na visa vya wapiga kura kurubuniwa kwa shilingi mia moja kile ambacho alikitaja kwamba ni kutokana na umaskini ambao uliwafanay watu kukubali kiasi hicho cha pesa ambacho ni sawa na pakiti nusu ya unga.

“Nadhani nitastaafu baada ya hili, Lakini nitabaki Kenya kwa sababu ni nchi yangu ninayoipenda na nitafia hapa. Lakini nitajitolea muda zaidi kwa mimi kusafiri kidogo kidogo niwezavyo kuona ulimwengu na hatimaye katika miaka michache ijayo nitastaafu,” alisema Esposito.

Aidha, mwanasiasa huyo alisema kwamba alikuwa na manifesto nzuri yenye kuzingatia zaidi elimu kwa sababu aligundua katika eneo hilo la pwani watu wengi hawana elimu ya kusoma wala kuandika na ndio ajenda yake kuu angechaguliwa kama rais wa kaunti na sasa kuwataka waliochaguliwa kuhakikisha wanawafanyia wananchi kazi haswa kuhakikisha wanapata elimu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved