Gavana mteule wa Makueni Mutula Kilonzo Junior amesema kumbukumbu wa rais anayeondoka Uhuru Kenyatta utategemea pakubwa jinsi atakayomkabidhi mamlaka yule atakaye mfuata kama rais.
Katika mahojiano na moja ya vyombo vya habari, Mutula alisema rais Kenyatta anafaa kujitokeza na kuwahakikishia Wakenya kuhusu uridhi wa amani.
“Kama ningekuwa Uhuru ningetoka nje, tumwone juu ya gari lake. Na aonekane mwenye furaha, kana kwamba hana wasi wasi. Yeye ndiye rais anayeondoka na hakuna mtu ambaye angejiuliza Uhuru yuko wapi,” Mutula alisema.
Rais Kenyatta amekaa kimya kufuatia matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9 ambapo naibu wake William Ruto alishinda mgombea wa urais Raila Odinga ambaye alikuwa akiwania kupitia tiketi ya Azimio La Umoja One Kenya.
Odinga na walalamishi wengine wanane walienda Mahakama ya Juu zaidi ili ushindi huo ufutiliwe mbali.
Rais Kenyatta alikutana na viongozi wa dini katika Ikulu, ambapo aliwahakikishia kuwa shughuli za mpito huo utakuwa mwepesi.
“Kuna wakati tulikuwa na mkutano kuhusu BBI na tulikuwa katika Ikulu na nilimwambia rais kwamba kumbukumbu wake mkubwa atakayoiacha sio BBI au barabara nzuri. Nilimwambia kwamba kumbukumbu wake mkubwa ni wakati atakapokabidhi mamlaka kwa amani,” Mutula
Mutula aliongeza kuwa rais anafaa kuwa mtulivu na si mtu mwenye wasi wasi , na pia kuhakikisha kuwa Kenya inazidi kudumisha amani.