Rais mteule William Ruto anatarajiwa katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta (KICC) kwa Kuapishwa kwa gavana mteule wa Nairobi Johnson Sakaja.
Ruto ni miongoni mwa wageni wanaotarajiwa katika hafla ya kuapishwa kwa gavana huyo.
Wabunge wote 17 waliochaguliwa wa Nairobi, Wabunge 84 wa Bunge la Kaunti, Seneta na Mwakilishi wa Wanawake pia watahudhuria.
Spika anayeondoka Benson Mutura pia atatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.
Ofisi ya Gavana imesema maandalizi ya hafla hiyo yamekamilika na kuwahakikishia wakaazi kwamba mabadiliko kutoka kwa utawala wa Anne Kananu yatakuwa laini.
Sherehe ya kuapishwa itafanyika kati ya saa 10 asubuhi na saa 2 jioni katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Kenyatta (KICC) kwa sababu Uhuru Park, ambayo imekuwa maeneo ya kufanya sherehe hizo,inafanyiwa ukarabati.
Magavana wa awamu ya pili kama vile Ayang Nyongo wa Kisumu na Mutahi Wahiga wa Nyeri walidhihirisha imani katika kuboresha utoaji wa huduma.
Jaji Mkuu Martha Koome tayari amewateua majaji watakaosimamia sherehe za kuapishwa.
Hakutakuwa na sherehe kama hizo katika kaunti za Mombasa na Kakamega baada ya IEBC kusogeza uchaguzi wa ugavana hadi Jumatatu.
Nassir atakuwa akipambana na Hassan Omar Sarai wa (UDA),ambaye ni mpinzani wake wa karibu katika kinyanganyiro cha kuwa gavana wa kaunti ya Mombasa, huku Cleophas Malala wa (UDA) akipambana na Farndanes Barasa wa (ODM) katika kinyanganyiro ya ugavana katika kaunti ya Kakamega .