logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Khalwale ampongeza Barasa baada ya kushinda kiti cha ugavana wa Kakamega

Barasa alipata kura 192,929 dhidi ya Malala aliyepata kura 159,508.

image
na Radio Jambo

Uchaguzi30 August 2022 - 12:50

Muhtasari


  • Khalwale ampongeza Barasa baada ya kushinda ugavana wa Kakamega
  • Alishinda katika majimbo yote ya kanda ya kusini na mengine mawili ya kanda ya kaskazini
Seneta wa zamani wa Kakamega Boni Khalwale

Seneta wa Kakamega Boni Khalwale amempongeza mgombeaji wa kiti cha ugavana wa ODM Fernandes Barasa baada ya kushinda kiti cha ugavana wa Kakamega.

Khalwale kwenye tweet alisherehekea gavana mteule na kumpongeza Cleophas Malala wa ANC kwa kupigana vilivyo.

"Hongera Barasa Fernandes kwa ushindi wako na Cleophas Malala kwa pambano lako la moyo," Khalwale aliandika.

Barasa alipata kura 192,929 dhidi ya Malala aliyepata kura 159,508.

Alishinda katika majimbo yote ya kanda ya kusini na mengine mawili ya kanda ya kaskazini.

ODM sasa imeshinda viti tisa kati ya 12 vya ubunge na 48 kati ya viti 60 vya MCA huko Kakamega.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved