logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jinsi udanganyifu, utakatishaji takwimu ulivyofanyika katika kura za Agosti - Orengo

• “Tunawaomba mbatilishe uchaguzi kwa msingi kwamba mshtakiwa wa pili hakupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa,” alisema. • Orengo ambaye pia ni gavana wa Siaya alisema IEBC haina utendakazi na haina uwezo wa kusimamia uchaguzi.

image
na

Habari31 August 2022 - 10:04

Muhtasari


• “Tunawaomba mbatilishe uchaguzi kwa msingi kwamba mshtakiwa wa pili hakupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa,” alisema.

• Orengo ambaye pia ni gavana wa Siaya alisema IEBC haina utendakazi na haina uwezo wa kusimamia uchaguzi.

Gavana wa Siaya James Orengo katika mahakama ya Juu mnamo Agosti 31,2022.

Tofauti na chaguzi nyingi, katika huu maalum, kulikuwa na udanganyifu na utakatishaji wa takwimu, Wakili James Orengo amesema.

Wakili mkuu na Gavana wa Siaya walisema hayo wakati wa kusikizwa kwa ombi la rais katika Mahakama ya Juu Jumatano.

Orengo, anayewakilisha Raila Odinga wa Azimio na Martha Karua, alisema mifumo ya IEBC ilipangwa kimbele.

"Utaratibu huu uliwezekana kwa shambulio la muundo wa IT na mfumo wa tume ya uchaguzi. Jinsi walivyoshughulikia fomu hizo zilipopakiwa na kupakuliwa,” alisema.

Orengo alisema baadhi ya fomu ziliandaliwa na kufutwa, kulingana na hati za kiapo.

"Tunaomba kubatilishwa kwa uchaguzi kwa msingi kwamba mshtakiwa wa pili hakupata zaidi ya asilimia 50 ya kura zilizopigwa," alisema.

Alisema IEBC haina utendakazi na haina uwezo wa kusimamia uchaguzi.

"Tuna tume ambayo imegawanyika katikati, ambayo inazungumza na chombo cha kikatiba kisichofanya kazi ambacho hakina uwezo wa kusimamia uchaguzi ambao utaipa uhalali ambao uchaguzi unahitaji."

Orengo alisema hadithi inayoibuka kutokana na matukio yaliyotokea wakati wa uchaguzi inakwenda kinyume na vipengee vilivyowekwa kwenye katiba.

"Malalamiko haya tunayoweka mbele yenu sio nadharia ya njama, sio tukio lolote la kawaida," alisema.

"Ushahidi uliowekwa mbele yako, kile kilichotokea na matukio yaliyofuata ni mfano wa ukiukwaji wa katiba ili kudhoofisha matakwa ya watu."

Orengo alisema, kama ilivyokuwa mwaka wa 2017, IEBC haikuongoza uchaguzi kama ilivyokusudiwa na katiba.

Timu ya mawakili ya Raila iliwasilisha kesi ikidai kuwa timu inayomfanyia kazi Rais mteule William Ruto iliingilia mfumo wa uchaguzi na kubadilisha picha halisi za fomu za matokeo ya vituo vya kupigia kura na kuweka za uwongo, hivyo basi kuongeza kura za Ruto.

Ruto alikanusha madai hayo katika hati ya kiapo aliyowasilisha mahakamani.

IEBC pia iliwasilisha majibu, huku makamishna watatu wakiunga mkono mchakato huo na wanne wakihoji.

Siku ya Jumanne, Mahakama ya Juu ilitoa maswali manane ambayo itayajibu itakapotoa uamuzi kuhusu matokeo ya uchaguzi wa urais ya mwezi huu yenye utata.

Mahakama iliunganisha maombi yote saba ya kupinga ushindi wa Ruto kuwa moja.

Benchi la majaji saba wanaosikiliza ombi hilo ni pamoja na; Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, Majaji Ibrahim Mohamed, Isaac Lenaola, William Ouko, Smokin Wanjala na Njoki Ndungu.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved