logo

NOW ON AIR

Listen in Live

(+Video) Wajackoyah amfokea shabiki aliyeshika sehemu zake za siri

"Usinishike hivyo!"... sasa huyu ananishika sehemu yangu ya nyeti!" Wajackoyah alisema.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri30 July 2022 - 08:43

Muhtasari


•Wajackoyah alilazimika kusimamisha hotuba yake kwa muda baada ya mfuasi wake mmoja aliyesisimka kugusa sehemu zake za siri.

•Wanamitandao walifanya mzaha na tukio hilo wakidai kuwa huenda shabiki huyo aliamua kufuata kauli mbiu ya Root Party chake Wajackoyah,  'Tingiza miti'.

Unyanyasaji wa kingono sasa unaonekana kumuathiri mtu yeyote bila ubaguzi wakiwemo wagombea urais.

Siku ya Ijumaa mgombea urais wa Roots Party Profesa George Wajackoyah alilazimika kusimamisha hotuba yake kwa muda baada ya mfuasi wake mmoja aliyesisimka kugusa sehemu zake za siri.

Wajackoyah ambaye alikuwa amevalia suruali ya michezo, T-shati ya kijani na durag kichwani kama ilivyo kawaida yake alikuwa amesimama juu ya lori huku akiwahutubia wafuasi wake wakati tukio hilo lilitokea.

"... na mimi nimekuja nikasema.." Wajackoyah alisikika akisema katika klipu ya video inayosambaa kabla ya mguso wa ghafla kwenye sehemu zake za siri kumsimamisha.

"Usinishike hivyo!"... sasa huyu ananishika sehemu yangu ya nyeti!" mgombea urais huyo ambaye alionekana kukerwa na kitendo hicho alisikika akilalamika.

Video ya tukio hilo imesambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii huku wanamitandao wakitoa hisia mseto.

Baadhi ya wanamitandao walifanya mzaha na tukio hilo wakidai kuwa huenda shabiki huyo aliamua kufuata kauli mbiu ya Root Party chake Wajackoyah,  'Tingiza miti'.

Haya baadhi ya maoni ya wanamitandao:-

@AtCheckmate Shabiki wa kike wa Wajackoyah mwenye kiu aliamua kuweka kauli mbiu yake ya TINGIZA MITI kwa vitendo kwa kumtikisa mwenye kauli mbiu “miti” YAWA!!??

_law_____ 😂😂ali kua ana angalia kaaa herb iko apo

lushy_puffy_254 Anaskizia penye Roots zinatoka 😂😂😂😂😂😂😂

mrbradley__  Tingiza tingiza

steveranker  😂😂😂😂Anataka kucastrate the 6th

trapkidobreezy Tabia mbaya inafanyika kila mahali😂😂

Haya yalijiri siku moja tu baada ya mgombea urais huyo na mgombea mwenzake Justina Wamae kuonekana katangamana na wafuasi wao katika klabu moja jijini Nairobi.

Picha zinazoonyesha wakiwa wamezingirwa na vipusa warembo zilisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kuwasisimua wanamitandao.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved