logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Nilihisi sitaki mahusiano na mtu maarufu baada ya kutengana na Otile Brown- Vera afunguka

Baada ya kujuana na Mauzo,  Vera aligundua kuwa mwimbaji huyo ni mwanaume tofauti.

image
na Samuel Maina

Vipindi14 October 2022 - 08:51

Muhtasari


  • •"Tulikutana na Brown Mauzo nikiwa na ex wangu. Baadae tulikutana nikiwa single na yeye alikuwa single," Vera alisema.
  • •Pia alidokeza kuwa mumewe hakuwahi kuwa kwenye mahusiano na Amber Ray kama inavyoaminika na wengi.
katika studio za Radio Jambo mnamo Oktoba 14, 2022.

Mwanasoshalaiti Vera Sidika amefichua kwamba alikuwa amekataa tamaa ya kujitosa kwenye mahusiano na mtu maarufu.

Katika mahojiano na mtangazaji wa Radio Jambo Massawe Japanni, Vera alisema kuwa hakutazamia kuchumbiana na msanii mwingine yeyote baada ya mahusiano yake na Otile Brown kugonga mwamba mwakani 2018.

"Nilihisi sitaki kuwa na mahusiano na mtu ambaye ni maarufu!" alisema.

Vera hata hivyo alikutana na mwimbaji Brown Mauzo miezi kadhaa baada ya kutengana na Otile Brown na kuwa marafiki.

Alifichua kuwa wakati alipokutana na mumewe kwa mara ya kwanza alikuwa anachumbiana na mwanaume mwingine.

"Tulikutana na Brown Mauzo nikiwa na ex wangu. Baadae tulikutana nikiwa single na yeye alikuwa single," alisema.

Mwanasoshalaiti huyo mwenye umri wa miaka 33 alisema yeye na Mauzo walikuwa marafiki kwa miezi kadhaa kabla ya kuanza kuchumbiana.

Baada ya kuwa kwenye urafiki kwa muda na kufunguka kuhusu maisha yao, Vera aligundua kuwa mwimbaji huyo ni mwanaume tofauti.

"Niliona ni mtu tofauti. Brown hata hajawahi kunywa pombe. Tulikuwa tunapigiana simu na kuongea kutoka  saa  tatu usiku  mpaka saa kumi na moja asubuhi. Tulikuwa marafiki. Tulikuwa wazi sana," alisema.

Vera alisema wakati alipojitosa kwenye mahusiano na Brown Mauzo, msanii huyo kutoka mkoa wa Pwani alikuwa ametengana na baby mama wake takriban miezi nane ambayo ilikuwa imepita.

"Mimi nilikuwa nimeachana na ex wangu takriban miezi saba iliyokuwa imepita," alisema.

Mwanasoshalaiti huyo pia alidokeza kuwa mumewe hakuwahi kuwa kwenye mahusiano na Amber Ray kama inavyoaminika na wengi.

"Wakati wa mahusiano yake ya awali, alikuwa akifanya kiki na mtu maarufu (Amber Ray). Hiyo kiki ikifanyika alikuwa kwenye mahusiano," alisema.

Miaka miwili na miezi mitano imepita sasa tangu wasanii hao wawili walianza kuchumbiana. Vera ameweka wazi kuwa anafurahia ndoa yake.

Amesisitiza kuwa amekuwa mwaminifu katika ndoa yake na hata hana uhusiano wowote na wapenzi wake wa zamani.

"Mimi nikiwa kwenye mahusiano huwa mwaminifu. Huwa sicheat. Wapenzi wangu wa zamani wanajua," alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved