Collins Kiplangat ,34, kutoka Kericho alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Stella Wanyama ,38, ambaye alikosana naye takriban wiki mbili zilizopita.
Kiplangat alisema mahusiano yao ya miaka mitatu yalisambaratika baada ya mpenziwe kupewa fitina kuwa ana wapenzi wengi. Alisema Stella pia alipata taarifa kuwa Kiplangat anatoka kijiji kimoja na aliyekuwa mpenzi wak, jambo ambalo hakupenda.
“Tulijuana kupitia simu. Kuna rafiki yake alinipatia namba yake akaniambia niongee nay eye kwa sababu ni mzee kumliko. Stella aliniambia anataka kuolewa hataki mtu wa mchezo. Aliniuliza kama nimewahi kuoa tena nikamwambia nilipata mtoto na msichana mwingine lakini sikuwa nimeoa,” Kiplangat alisimulia.
Aliongeza, “Juzi aligundua kuwa tunatoka kijiji moja na yule kijana ambaye alinipatia namba yake. Alisema anataka kutoa mimba kwa sababu natoka kijiji na huyo kijana na kwa sababu ya zile hadithi alisikia. Aliambiwa ati niko na wanawake wengi. Hata tulikuwa tuende kwetu nilikuwa nimesema nyumbani kabla ya mambo hayo kutokea.”
Kiplangat alibainisha kwamba hana shida yoyote na umri wa mpenziwe licha ya kuwa ni mzee kumshinda.
“Sasa hizi yuko kwa roho sijui nifanye nini. Amekataa mimi na nimemuweka kwa roho,” alilalamika.
Stella alipopigiwa simu alisikika kustaajabishwa na hatua ya Kiplangat kuomba kupatanishwa na yeye kwa radio.
“Ambia yeye anivumilie nitampigia asiniweke kwa radio madaktari wenzangu wanaweza kunisikia,” Stella alisema kabla ya kukata simu mara moja.
Kiplangat alithibitisha kuwa mpenzi huyo wake ni daktari wa upasuaji katika moja ya hospitali kubwa nchini na kueleza jinsi alivyokuwa amefurahi kumfanya mkewe.
“Hapo nilikuwa nimeangukia bibi kabisa. Nilikuwa nimeona shida zangu zote zimeisha kabisa mpaka nikasema Mungu si adhumani kabisa. Nilikuwa nimeona nimeangukia jackpot,” alisema.
Kiplangat alisema hofu yake kubwa ni mwanamke huyo kutoa mimba ya mtoto wao kama alivyotishia. Alisema Stella alikuwa na ujauzito wa miezi miwili wakati alipomuacha.
“ Kitu inaniuma ni kuwa alisema ataua mtoto wangu,” alisema.
Juhudi za kuwapatanisha wawili hao hata hivyo ziligonga mwamba kwa kuwa Stella alizima simu yake.