Tukio la kushangaza lililowaacha waumini vinywa wazi washindwe cha kufanya baada mama mkongwe kufika madhabahuni na kumzaba kofi mchungaji aliyekuwa akihubiri huku akidai ujumbe huo unamuhusu sana na pasta alikuwa akihubiri mambo yake kanisani.
Mama huyo mkongwe alidai muhubiri huyo alikua akimsimanga kwa kuhubiri ukweli kuhusu matendo yake ambayo yeye huyafanya.
Kulingana na Gidi kwenye Radio Jambo alieleza kwamba Mchungaji huyo hakua anamfahamu mama huyo na wala hakuwa na ushuhuda wowote kumuhusu kwa hivyo hakuwa na hatia.
"Katika yale mahubiri, pastor huwa anazungumza na kuhubiri na wakatimwingine huwa wanaguza maisha yetu. Sasa inasemekana siku ya jumapili hapa Kangundo ukambani, pasta alianza kuzungumza kuhusu dunia vile imepasuka. Akasema wanaume weingi sana siku hizi wana mipango ya kando, akaendelea na akasema kina mama pia wana mipango ya kando na waume wa watu,' alisema mchungaji huyo.
"Kulikuwa na ripoti hapo awali kwamba wanawake wengi kutoka maeneo ya ukambani wana zaidi ya wanaume watatu. sasa huyu pasta akaendelea kuhubiri na akaanza kusema wanawake wa huku ukambani wako na wazee wa watu. unapata mwanamke ana waze wanne. Na ule mama aliposikia alitoka kanisani kule nyuma, mama mzee mkongwe akaja mbele watu wanashangaa. Sasa kanisa ikanyamaza kungoja, alikuja akamzaba kofi pasta mbele ya watu na akasema unazungumza habari yangu,' alieleza Gidi.
Kwenye stori za Ghost, Gidi ameeleza kwamba mama huyo mkongwe alikasirika sana na mahubri hayo na akaamua kuondoka kanisani huku akiapa kutorudi tena hapo kanisani. Yule mama pia alimuzomea pasta kwa kuhubiri kumuhusu.
"Pasta akashtuka na watu wakabaki kimya. yule Mama akauliza nani anakwambia uongelee mambo yangu kanisani. Mama akatoka akasema inauma na nimetoka hii kanisa na akaenda. Waumini walibaki wameshangaa. Huyu mama ni kama alikuwa mhusika mkuu kwa ujumbe wa mhubiri," alisema mtangazaji Gidi.