'Naumia sana!Niko na woga!' Wanjiru, mama ya ndugu waliouawa Kitengela afunguka kuhusu anavyopambana na majonzi

Amesema kuwa imekuwa ngumu kupambana na majonzi yaliyomkumba baada ya msiba huo kumpata na kukiri kwamba anajihisi kuwa anahitaji sana huduma za wataalam wa kisaikolojia.

Muhtasari

•Wanjiru amesema kuwa kwa sasa anaumia sana na hawezi taka mtu mwingine apitie wakati mgumu kama anaopitia baada ya  kuwapoteza wanawe wa pekee.

•Mama huyo amesema kuwa alikuwa na uhusiano wa karibu sana na wanawe na aliwachukulia sio tu kama wanawe ila pia kama mumewe kuona kua walitengana na mumewe zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Bi Lucy Wanjiru katika studio za Radio Jambo siku ya Jumanne
Bi Lucy Wanjiru katika studio za Radio Jambo siku ya Jumanne
Image: RADIO JAMBO

Mgeni wetu siku ya leo katika kipindi cha Bustani la Massawe kitengo cha 'Ilikuaje?' alikuwa Bi Lucy Wanjiru ambaye ni mama ya ndugu wawili waliouawa mjini Kitengela takriban wiki tatu zilizopita.

Siku chache baada ya kuzika wanawe marehemu Fredrick Muriithi (30) na Victor Mwangi (25) nyumbani kwao maeneo ya Nyahururu , Bi Wanjiru ameendelea kutoa ombi haki itendeke haraka ili aweze kupata utulivu wa moyo.

Wanjiru amesema kuwa kwa sasa anaumia sana na hawezi taka mtu mwingine apitie wakati mgumu kama anaopitia baada ya  kuwapoteza wanawe wa pekee.

"Naumia sana.. ombi langu kwa serikali nataka haki itendeke kwa kuwa watoto wangu hawapo tena. Kama tunaweza kupata haki ya watoto tunaweza kufurahi sana.. ningependa serikali wanisaidie kupata haki na tena kusipatikane jambo kama hilo tena. Nimeskia uchungu sana na naomba kusiwe na mtu mwingine atakayepitia jambo kama hilo.Kama hii kitu inaweza kumalizika kabisa, mimi nimeumia kabisa na niko na machungu. Kusipatikane mtu mwingine atalia jinsi nimelia. Haki ikapatikana naweza furahi sana" Bi Wanjiru aliambia Massawe.

Mama huyo amesema kuwa alikuwa na uhusiano wa karibu sana na wanawe na aliwachukulia sio tu kama wanawe ila pia kama mumewe kuona kua walitengana na mumewe zaidi ya miaka 20 iliyopita.

Amesema kuwa imekuwa ngumu kupambana na majonzi yaliyomkumba baada ya msiba huo kumpata na kukiri kwamba anajihisi kuwa  anahitaji sana huduma za wataalam wa kisaikolojia.

Wanjiru amesema kuwa kwa sasa anaishi na hofu kubwa na mara kwa mara anajipata akipiga nduru usiku haswa anapowaza kuhusu walichokipitia wanawe mikononi mwa wauaji.

"Kuna watu wengi ambao wanakuja kuniangalia na kuniongelesha lakini ningetaka tu mtu ambaye anaweza kunishauri na maombi sana kwani nahitaji maombi sana na mashauri. Kuna kitu inanipata usiku nikifikiria vile wanangu walihisi uchungu mwingi walipokuwa wanauawa, walivyolilia huruma. Nafikiria vile watoto walipigwa wakiona wanauliwa. Jana hata nilipiga nduru usiku 

Niko na uwoga sana! Uwoga ni mwingi! Hata hivo tunamuomba Mungu uoga uishe.. Niko na uwoga kwa sababu hatujajua kiini cha hawa watoto kuuliwa ni nini. Sijawahi kuwa na ugomvi na mtu lakini najiuliza kwa nini na kwa nini ilifanyika hivo. Nahisi kama kwamba ni njama.. Hiyo uoga lazima iishi ndani yako kila wakati kwa sababu ni maswali ambayo hana majibu.. Najiuliza mbona?" Bi Wanjiru aliambia Massawe. 

Wanjiru ameeleza kwamba moyo wake ulivunjika alipoona miili ya wanawe katika chumba cha kuhifadhi maiti cha KU na kusema kuwa wanawe walikufa kifo cha uchungu sana kuona kuwa mili yao ilikuwa na ishara za kudungwa kila mahali.

"Ilikuwa wakati mgumu kwangu. Vile nilitazama niliona kuwa ni wao kweli.. Kusema kweli mimi niliona watoto wangun walipata kifo cha uchungu sana sababu walikuwa wamedungwa kila mahali. Walikufa na uchungu sana." Wanjiru alisema.

Amesema kuwa alipoteza fahamu punde baada ya kutazama mili ile na fahamu yake ilirejea tu baada ya kupata matibabu katika hospitali ya Kenyatta